Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi amemtunuku Nishani ya Mapinduzi Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa  amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, Tanzania na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla ya kutunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein,iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar,Tanzania na wa Afrika Mashariki katika hafla ya kutunuku kwa Nishani ya Mapinduzi na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdalla.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha Nishani ya Mapinduzi Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, baada ya kumtunuku Nishani ya Mapinduzi, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2022.(Picha na Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akibadilishana mawazo na  Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) mara baada ya kumtunuku nishani ya Mapinduzi  katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi. [Picha na Ikulu] 11/01/2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein mara baada ya kumtunuku nishani ya Mapinduzi  hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ikulu] 11/01/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.