Habari za Punde

Tudumishe usafi maskulini ili kuepukana na maradhi

 Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu Zanzibar bi Asya Iddi Issa akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira mmoja wa Maafisa elimu Wilaya na Mikoa katika ukumbi wa wizara ya Elimu Mazizini Unguja.

 Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu Zanzibar bi Asya Iddi Issa alipokuwa akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Maafisa elimu Wilaya na Mikoa katika ukumbi wa wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Baadhi ya vifaa vya usafi wa mazingira ambavyo walikabidhiwa Maafisa elimu Wilaya na Mikoa katika ukumbi wa wizara ya Elimu Mazizini Unguja.


Na Maulid Yussuf , Wema

 Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu Zanzibar bi Asya Iddi Issa amesema ipo haja ya kudumisha usafi katika Skuli zote ili kuepukana na maradhi mbalimbali.

Amesema hayo wakati wa hafla ya kuwakabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Maafisa elimu Wilaya na Mikoa katika ukumbi wa wizara ya Elimu Mazizini Unguja.
Amesema kutokana na wingi wa Skuli Wizara imeamua kukabidhi vifaa hivyo kwa baadhi ya Skuli kwa ajili ya watoto wa msingi, ikiwa lengo ni kuhakikisha wanapambana na maradhi hasa ya UVIKO 19.
Jumla ya skuli za msingi 110 zimekabidhiwa vifaa hivyo zikiwemo Wilaya ya Kaskazini A' Skuli 16, Wilaya Kaskazini B' 16, Wilaya ya Kusini Skuli 16, Wilaya ya kusini 16, na Wilaya ya kati 16 ambapo Wilaya ya Magharib A" Skuli 15 na Wilaya ya Magharib B" Skuli 15.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na sabuni, detol, taula za kike pamoja na vifaa vyengine vya usafi ambavyo vimetolewa na Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNICEF) kupitia mradi wa (wash) ukiwa na lengo la kumlinda mtoto awe katika mazingira salama na kuhakikisha mtoto wa kike anapata siku zake salama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.