Habari za Punde

Mradi wa utafiti wa samaki kusaidia maendeleo ya uchumi wa buluu


 MKURUGENZI MKUU wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Bahari Dkt. Zakaria Ali Khamis kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi amesema mradi wa utafiti wa samaki utasaidia kuimarisha azma ya Serikali katika maendeleo ya uchumi wa buluu hapa Zanzibar.

Dkt. Zakaria amesema hayo baada ya kufungua mafunzo ya utafiti wa mradi wa samaki kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali vya Tanzania na Chuo cha Norway.

Dkt. Zakaria amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu vya SUZA na chuo kikuu cha Dar-es-Salaam kupitia mradi huo katika kusaidia na kushirikisha jamii hususani wanawake katika shughuli za uvuvi.

Sambamba na hayo dkt. Zakaria amesema utafiti wa samaki utabainisha madhara yaliomo katika rasilimali za bahari kutokana na wananchi wengi wanategemea protini na lishe bora zinazotokana na samaki.

Prof. Ina Baryceson kutoka WIOMSA amesema kupitia usalama wa chakula na lishe tafiti za rasilimali za bahari katika maabara zinalenga maisha ya watu kwa jinsia zote nchini na maendeleo kwa Serikali.

Dr. Julius Francis kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam amesema kufanya tafiti sio kitu cha muda mfupi hivyo ni vyema kujuwa kwamba kwanza lazima kujenga misingi bora ambayo sio ya muda mfupi.

Dr. Julius amesema mradi wa samaki ambao unatekelezwa kwa mashirikiano baina ya vyuo vya Norway na Tanzania kunahitaji kutolewa taarifa za kutosha ili kuwa mradi bora zaidi.

Mkutano huo umefanyika kwa mashirikiano ya chuo kutoka Norway, chuo cha Dar-es-Salaam, SUZA pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Rasilimali za Bahari Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.