Habari za Punde

Mwalimu Ali Harith Bakari atunukiwa cheti cha Shukurani

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Ali Khamis Juma akimkabidhi cheti cha shukurani Mwalimu Ali Harith Bakar kutokana na mchango wake wa kujitolea kutoa mafunzo kwa Walimu wanaofundisha somo la kiswahili katika Skuli za sekondari na kupelekea Zanzibar kuwa ya kwanza Kitaifa kwa somo hilo kwa kidato cha nne.
Tukio hilo limefanyika huko ofisini kwake Mazizini Unguja (wa kwanza kushoto ) ni Mkurugenzi Ofisi ya Mkaguzi wa Elimu bi Maimuna Fadhili Abass ambae wakati huo alikuwa ni Mkurugenzi idara ya Mafunzo ya ualimu Wizara ya Elimu Zanzibar na wa (kwanza kulia) ni mshauri wa somo la kiswahili Taifa bi Asha Said Nassor.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.