Habari za Punde

Mhe. Rais Samia apokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Malawi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Malawi hapa nchini Mhe. Andrew Posyantos Efron Zumbe kabla ya kupokea Hati yake ya Utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo tarehe 29 Machi, 2022.

Balozi wa Jamhuri ya Malawi hapa nchini Mhe. Andrew Posyantos Efron Zumbe akiwasilisha Hati yake ya Utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo tarehe 29 Machi, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Malawi hapa nchini Mhe. Andrew Posyantos Efron Zumbe mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo tarehe 29 Machi, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Malawi hapa nchini Mhe. Andrew Posyantos Efron Zumbe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dodoma leo tarehe 29 Machi, 2022
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.