Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Dr. Maxime Ikulu Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dr. Maxime Houinato, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yaliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dr. Maxime Houinato, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yaliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dk.Maxime Houinato baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kujitambulisha. na (kushoto kwa Rais) Mwakilishi wa UN Women Bi. Hodan Addou.

Mkurugenzi wa UN WOMEN Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Dk. Maxime Houinato akiwa amefuatana na ujumbe wake alifika Ikulu Zanzibar kuzungumza na Rais Dk. Mwinyi ambapo alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa jinsi anavyozingatia suala zima la usawa wa kijinsia katika uteuzi wake wa viongozi.

Mkurugenzi huyo pia, aliahidi kwamba UN WOMEN itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mikakati yake ya kuwaunga mkono wanawake katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nae Rais Dk. Mwinyi kwa uapnde wake alimuelezea kiongozi huyo mikakati mbali mbali iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakaikisha wanawake na watoto wanapata haki zao za msingi.

Aidha, alieleza hatua zilizowekwa na serikali anayoiongoza katika kuwawezesha wanawake.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.