Afisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz Said Ali akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Lipa kwa Simu ambayo inayowaruhusu wateja kulipia bidhaa na huduma kwa njia ya simu.Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kifedha, Moses Alphonce.
Aliyekuwa
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akifanya manunuzi kwa
mfanyabiashara Zuena Ali maarufu kama Manjua Doux wakati wa uzinduzi wa huduma
ya Lipa kwa Simu.Kulia kwake ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz Said Ali na
Mkuu wa Huduma za Kifedha, Moses Alphonce.
Balozi wa
Kampeni ya Lipa kwa Simu, Mau Mpemba akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma
ya Lipa kwa Simu.Kushoto ni Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz Said Ali na Mkuu wa
Huduma za Kifedha, Moses Alphonce.
Katika kuboresha huduma za malipo kidigitali, kampuni ya Zantel leo imezindua huduma yake ya Lipa kwa Simu ambayo itawaruhusu wateja kulipia bidhaa na huduma moja kwa moja kutoka kwenye simu kwenda kwa wafanyabiashara.
Huduma hiyo itachochea
maendeleo na matumizi ya teknolojia kwenye huduma za malipo kwenye sekta zote
za kiuchumi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi, Afisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz Said Ali alisema huduma
hiyo itasaidia katika kuongeza ufanisi
kwa wafanyabiashara pamoja na kuongeza usalama wa fedha kwa wananchi.
“Huduma hii inaenda kuboresha malipo kuwa ya
kidigitali zaidi hapa Zanzibar kwani wateja wataweza kulipia bidhaa na huduma
kwa kulipa moja kwa moja kutoka kwenye simu zao.Hii inaondoa ulazima wa kubeba
pesa taslimu ambazo usalama wake ni mdogo,” alisema.
Zantel inakuwa kampuni ya kwanza kwa Zanzibar
kuanzisha huduma hiyo ambayo ni huduma kamili ya kidigitali inayowaruhusu
wateja kulipia kutoka mitandao mingine.
“Tuna wafanyabiashara zaidi ya 4,000 ambao
wanatoa huduma hii kote Unguja na Pemba na tunaendelea kusajili wafanyabiashara
wengi Zaidi ili huduma hii ipatikane kila kona ya Zanzibar,”
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza ajenda ya Uchumi wa Bluu ambayo imejikita katika matumizi ya kimkakati ya rasilimali maji ili kuchangia ukuaji wa uchumi.Huduma hii itasaidia kurahisisha ukuaji wa biashara kwenye sekta kama uvuvi na utalii.
Mkuu wa Huduma za Fedha wa Zantel, Moses
Alphonce alisema huduma hiyo ni rahisi kutumia na hivyo kampuni hiyo inaendelea
na utoaji wa elimu kwa wananchi ili waelewe umuhimu wake.
“Ili Kulipa kwa Simu, unachotakiwa kufanya ni
kwenda kwenye menyu ya huduma za fedha ya mtandao wako na kufuata maelekezo.Kwa
watumiaji wa simu janja wanaweza kulipa kwa ku-scan QR code kwenye App ya
Ezypesa,”
Wateja wa
Ezypesa watapiga *150*02# na kuchangua 5 Lipa kwa Ezypesa, kisha ingiza Lipa
Namba Kisha ingiza kiasi na thibitisha kwa kuweka Pin yako.
Huduma hiyo
tayari inapatikama kwenye maeneo mbalimballi ikiwamo Migahawa, hoteli, masoko,
supermakets, maduka yad awa, vituo vya mafuta, na maeneo ya wazi kama
Forodhani.
No comments:
Post a Comment