Habari za Punde

Kinana Awataka Wabunge na Madiwani Kutopitisha Sheria Zinazominya Haki na Kuwabana Wananchi.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Abdulrahmana Kinana akifurahia nyimbo ya Kikundi cha ngoma ya Asili ya Watu wa Mwambao alipowasili Mkoani Tanga kwa ziara ya Kichama.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka  madiwani na wabunge kukataa  kupitisha miswada ya Sheria  yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka  kulitazama vyema  kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.

"Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.

"Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano...sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane  na wananchi," alisema.

Balozi wa Zaidi ya Miaka 25 katika tarafa ya korogwe mjini Ndg Mika M Mwirongo  akifurahi kumuona Makamu Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi Bara Comrade Kinana kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe.
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiteta jambo la Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi
Makamu Mwenyekiti CCM bara comrade Abdulrahman Kinana akimsikiliza Katibu wa  waendesha Bodaboda wa mjini Korogwe  Ndg Said mara baada ya kikao chake na wana ccm wa mkoa wa Tanga mjini humo.
Makamu Mwenyekiti CCM Bara comrade Abdulrahman Kinana kizungumza na mama mjasiriamali aliyekuwa akiuza bidhaa zake nje ya ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe ambako Kinana alifanya mkutano na wanachama na viongozi wa Chama hicho mkoa wa Tanga.
Makamu mwenyekiti wa CCM bara Comrade Abdulrahmana Kinana akizungumza na wanachama na wapenzi wa CCM wa Mkoa wa Tanga kwenye ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe akiwa kwenye ziara yake ya mikoa minne kukagua uhai wa chama.
Makamu mwenyekiti wa CCM bara Comrade Abdulrahmana Kinana akizungumza na wanachama na wapenzi wa CCM wa Mkoa wa Tanga kwenye ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe akiwa kwenye ziara yake ya mikoa minne kukagua uhai wa chama.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakimsiki8liza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Comredi Abdulraham Kinana akizungumza na WanaCCM , wakati wa ziara yake Mkoani Tanga.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakimsiki8liza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Comredi Abdulraham Kinana akizungumza na WanaCCM , wakati wa ziara yake Mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.