Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekabidhi Sadaka ya Futari kwa Wananchi Wenye Mahitaji Maalum Micheweni Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kulia)Mama Mariam Mwinyi, na (kushoto kwa Rais) Kiongozi wa Taasisi ya Miraji Tanzania Sheikh.Arif Suria, akizungumza na kuwasalimia Wananchi wenye Mahitaji Maalumu (Wazee,Watu wenye ulemavu na Mayatima) wakati wa hafla ya kugawa sadaka na futari iliyotolewa na Taasisi ya Miraji Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya mpira micheweni Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza haja kwa waumini wenye uwezo kuwasaidia wenzao wenye mahitaji maalum hasa katika kipindi hichi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akikabidhi sadaka ya futari kwa wananchi wenye mahitaji maalum katika maeneo ya Mkoani, Chanjanjawiri na Tibirinzi Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa ugawaji wa sadaka hiyo iliyotolewa na wafadhili mbali mbali wa ndani na nje ya Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wale wote waliosadakiwa kutokana na sadaka hizo za futari walizozitoa kwa wananchi wa kisiwa ha Pemba na hata Unguja.

Alimpongeza Bwana Suhail Muzamil ambaye ni msimamizi wa sadaka zilizotolewa na wafadhili kutoka nchini Kuwait pamoja na wafadhili kutoka Kampuni ya Olympic, Miraj na wengineo kwa uwamuzi wao wa kuwasidia ndugu zao futari hizo katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi ambae amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi katika zoezi hilo aliwataka waumini wenye uwezo hapa nchini nao wazidi kutoa sadaka zao kwa ndugu zao waumini wenye mazingira magumu.

Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kutoa shukurani za pekee kwa wale wote waliojitolea kuwasaidia ndugu zao sadaka ya futari katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kueleza kwamba amefarajika kutokana na mwamko mkubwa wa watoaji mwaka huu kwa upande wa Unguja na Pemba.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa niaba ya uongozi wa Wilaya ya Mkoani na Chake chake alitoa shukurani kwa Rais Dk. Miwnyi kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la ugawaji wa sadaka hiyo zoezi lililoanza tokea jana (12.04.2022) huko Mkoa wa Kaskazini Pemba..

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Taasisi ya Miraji Tanzania Sheikh.Arif Suria kuhusiana na Taasisi hiyo kutoa msaada kwa Wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi sadaka ya futari kwa Wananchi  wenye mahitaji maalum (Wazee,Watu wenye Ulemavu na Yatima (kulia kwa Rais )Mama Mariam Mwinyi,iliyofanyika katika viwanja vya mpira micheweni Pemba.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimkabidhi msaada wa Futari mmoja wa Wananchi wa Makundi Maalumu (Wazee,Watu Wenye ulemavu na Yatima) Bi.Time Hamad Ali, iliyotolewa na Taasisi ya Miraji Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya mpira Micheweni Pemba
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi  futari mmoja wa Wananchi wenye mahitaji maalumu Hamad Hussein Hamad, hafla hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Watoto Yatima Micheweni Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.