Habari za Punde

DC MOYO AMREJESHA MADARAKANI MWENYEKITI WA KIJIJI ALIYETIMULIWA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi ili kutatua mgogoro uliomuondosha madarakani mwenyekiti wa kijiji cha Ng'enza na hatimaye akamrudishia madaraka yake
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi ili kutatua mgogoro uliomuondosha madarakani mwenyekiti wa kijiji cha Ng'enza na hatimaye akamrudishia madaraka yake
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara ambao umerejesha madaraka ya mwenyekiti alikuwa amenyang'anywa madaraka yake ya uongozi wa kijiji
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara ambao umerejesha madaraka ya mwenyekiti alikuwa amenyang'anywa madaraka yake ya uongozi wa kijiji

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametengua maamuzi batili ya Serikali ya Kijiji Cha Ng'enza kata ya Magulilwa Wilayani humo yaliyomuondosha madarakani Bw. Angelus Mwigani aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho.

Mkuu wa Wilaya aliyefika Kijijini hapo baada ya kupokea malalamiko yaliyowasilishwa Kwa njia ya barua na Mwenyekiti huyo, Alisema utaratibu ulikiukwa ikiwemo kutokuwapo Kwa vikao Halali vya kumuondosha madarakani kiongozi huyo aliyechaguliwa na Wananchi.

Moyo alisema kuwa kuwa serikali ya kijiji hicho inajumla ya wajumbe 25 ambao wanaweza kutoa maamuzi yoyote ya serikali ya kijiji lakini katika kujadili swala la mwenyekiti walikuwepo wajumbe kumi na moja (11) jambo ambalo limesababisha kuondelewa mwenyekiti kwenye nafasi hiyo.

Alisema kuwa kweli amepokea malalamiko zaidi ya kumi na tisa (19) ambayo yanamkabili mwenyekiti wa kijiji hicho na hayapingi malalamiko hayo bali anachopinga ni namna ambavyo utaratibu uliotumika kumuondoa mwenyekiti kwenye nafasi ya uongozi.

Moyo alisema kuwa amemrejesha kwenye nafasi ya uongozi kwa kuwa Kikao kilichofanywa na wajumbe waliomuondosha hakikuwa kikao halali kwani mwenyekiti wa kikao hicho hakuwa miongoni mwa wajumbe huku akidi  haikutimia ili kufanya maamuzi

Alisema kuwa wajumbe wanatakiwa kurudi kwenye vikao halali ili kuweza kumuondosha mwenyekiti huyo kama wanataka kwa kufuata utaratibu unaotakiwa kama vile wajumbe kufikia robo tatu ya wajumbe,wapige kura au chama ndio kiamue kufuta uanachama.

Moyo alisema kuwa wakifuata sheria na taratibu zote za kumuondosha mwenyekiti yeye atenda tu kubali kuondolewa kwake kwa kuwa tayari mezani kwake anamalalamiko kumi na tisa (19) ambayo yanaweza kumuondosha mwenyekiti huyo.

Awali baadhi ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji walimueleza mkuu wa Wilaya kuwa maamuzi ya kumuondoa madarakani mwenyekiti kutokana na ubadhilifu wa mali za serikali ya kijiji cha Ng’enza na kutumia vibaya madaraka yake.

Walisema kuwa  mwenyekiti huyo amekuwa najiusisha na uuzaji wa mali za kijiji kwani aliuza miti bila idhini ya wajumbe,kula fedha za kijiji kiasi cha shilingi elfu sitini (60,000),kuongoza kwa vitisho wananchi ambavyo alikuwa anatumia vibaya madaraka yake.

Walisema kuwa waliamua kumuondosha madarakani baada ya kukiri kuwa amefanya makosa hayo na kusema kuwa atarusha baadhi ya fedha na kujirekebisha katika uongozi wake.

Waliongeza kwa kusema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa anagombana na mtendaji wa kijiji kila wakati kutokana na kutaka kutumia vibaya mali za serikali ya kijiji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.