Habari za Punde

Kampuni ya JHIL Enterprises Yapongezwa Kwa Ujenzi wa Kiwanja cha Kriket Fumba Zanzibar.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji wa Ujenzi wa Uwanja wa Kriketi Fumba Wilaya ya Magharibi “B”Unguja kutoka Nchini India ukiongozwa na Bw.Jilesh Hitmat Babla,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya JHIL Enterprises ya India, walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 2-6-2022, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe Tabia Maulid Mwita na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na mmoja wa Wawekezaji wa Uwanja wa Kriket Fumba kutoka India Bw.Zubin Karkaria CEO wa Kampuni ya VFS.Global, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 2-6-2022

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi ampongeza utayari wa Kampuni ya JHIL Enterprises kutoka India wa kujenga kituo cha Kimataifa cha michezo hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo Ikulu Zanzibar, alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Kampuni hiyo, ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni  Jilesh Himat Babla.

Katika pongezi hizo, Dk. Mwinyi ameshukuru Kampuni hiyo kwa utayari wake wa kujenga Kituo cha Michezo, kitakachohusisha Klabu ya kimataifa ya Kriketi pamoja na viwanja mbali mbali vya michezo (Indoor games) katika eneo la Uwezekezaji h Fumba, Wilaya Magharibi ‘B’ Unguja.

Alisema kwa kuzingatia kuwa Zanzibar ni kituo muhimu cha Utaliii, hatua ya ujenzi w akituo hicho ni muhimu katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar kimataifa pamoja na kukuza sekta ya michezo.

Nae, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  JHIL Enterprises Jilesh Himat Babla alimhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa kampuni hiyo itaendeleza mashirkianao na Serikali kupitia Wizara husika na kuhakikisha mradi huo unakamilika na kufikia malengo yaliowekwa ya kuutangaza utalii pamoja na kuimarisha sekta ya michezo hapa nchini.

Mapema, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita alisema mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kuwafaidisha wageni mbali mbali watakaozuru, watalii  pamoja na wazawa.

Ujumbe huo ulihusisha Wawekezaji pamoja na wachezaji waliopata kuwa maarufu katika mchezo wa Kriketi nchini India na nchi  yenginezo Barani Ulaya.

Katika hatua nyengine, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi huo unatakaofanyika kesho eneo la Uiwekezaji Fumba.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.