Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mhe.Hassan Khamis Hafidh (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi kitengo cha kinga na Elimu ya Afya Dkt Salim Slim wakati wa ziara ya kikazi katika vituo vya Afya kusisitiza utendaji wa kazi na utowaji wa huduma bora kwa Wananchi.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR.
Na Rahima Mohamed Maelezo 27/06/2022
Naibu Waziri wa afya Mhe.Hassan Khamis Hafidh amewataka wauguzi wanaoshughulikia miradi mbalimbali kurudi katika vituo vya afya ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo amesema katika ziara ya kuangalia utendaji kazi kwa vituo vya afya vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Mpendae na Sebleni Wilaya ya Mjini amesema kurudi kwa wauguzi hao itasaidia kuondoa usumbufu uliopo katika vituo hivyo.
Amesema amaegundua changamoto nyingi ikiwemo uchelewaji wa watendaji wa afya hali inayopelekea wananchi kusubiri muda mrefu kupata huduma.
Naibu Hassan ameeleza kuwa azma ya Serikali ni kuwapatia wananchi huduma bora hivyo watendaji wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kufuata sheria za kazi ili kuondosha usumbufu kwa wagonjwa wanaofika vituoni kupata huduma.
Aidha amesema Wizara haitosita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka majukumu yao na kusababisha uzoroteshaji wa huduma hiyo ili kuepusha malalamiko kwa jamii.
Nae Naibu Mkurugenzi wa Kinga wizara ya afya Salim Slim amesisitiza mashirikiano katika malezi kwa kina baba kuwapeleka watoto kliniki ili kujua maendeleo ya ukuaji wa afya za watoto wao.
Nao watendaji wa vituo hivyo wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vipimo vya kupimia damu kwa mama wajawazito,gari ya kubebea wagonjwa wa dharura,vikalio pamoja na uhaba wa eneo hali inayopelekea wagonjwa kukaa muda mrefu kusubiria huduma wanapofika vituon hapo.
No comments:
Post a Comment