Habari za Punde

Hafla ya uwekaji msingi kituo cha amali kwa wanafunzi wa kike Bungi


 Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Kuongezeka kwa Taasisi za Elimu na Ujuzi hapa Nchini Kutasaidia Kuongeza Fani na Taaluma kwa Wananchi kwakupata wataalamu tofauti.

  

Akizungumza katika uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo Cha Amali kwa Wanafunzi wa Kike huko Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.

 

Amesema hatua hiyo pia itasaidia Kupungua kwa hali ya Utegemezi Kwa kuwajengea Misingi bora  Miongoni Mwa Wananchi ikiwemo kujiajiri wenyewe 

 

 

Mhe. Hemed Amesema Kumekuwa na Taasisi Nyingi Zinazofanya kazi kwa Lengo la Kusaidia Serikali katika Sekta ya Elimu hivyo Amewaomba Wananchi Kuthamini Juhudi Hizo na kuwa Tayari katika kuona Lengo Hilo linafikiwa kwa Kujitokeza Kupata Elimu na fani zitakazowasaidia Kuwainua Kiuchumi.

 

 

Aidha ameipongeza Bodi ya MIF katika Kufanya Kazi kwa Kuzingatia Mahitaji ya Jamii   Kutokana na Umuhimu wa Elimu kwani Wameonesha Kipaumbele Zaidi kwa wasiokuwa na Uwezo,Wenye Ulemavu na Mayatima Jambo Ambalo Serikali Imekuwa ikihimiza ilo kuona Makundi Yote yananufaika.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation MIF Mhe. Wanu Hafidh Ameir amesema Watahakikisha wanaitunza misaada hiyo ya kielimu wanayopatiwa na U.A.E Kwani Inalenga kuwakomboa Wananchi kwa Maslahi ya Taifa.

 

Akitoa Salamu kutoka Umoja wa Falme za kiarabu Emirates (UAE) Waziri wa Nchi wa U.A.E) Sayyidah Maithaa Al Shaamy amesema Kukamilika kwa Kituo hicho Kutasaidia Kuwajengea Uwezo Wanafunzi wa Kike katika kuwakuza kitaalamu na kubadilisha Maisha Yao.

 

 

Katika Hafla hiyo  Pia Mhe. Hemed alishuhudia utiaji Saini wa ujenzi wa Chuo hicho cha Bungi Community Development kati ya Umoja wa Falme na Kiarabu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambapo wazo la ujenzi huo limetolewa na Taasisi ya MIF.

 

……….

Abdulrahim Khamis

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

04 Julai 2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.