Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mulembwa Munaku akizungumza na Ujumbe wa Benki ya
Dunia walipofika katika Ofisi za Wizara hiyo Agosti 2, 2022 na kufanya
mazungumzo kuhusu
maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.
UJUMBE
wa Benki ya Dunia jana Agosti 2, 2022 umetembelea Ofisi za Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, zilizopo jijini Dodoma na kufanya
mazungumzo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mulembwa Munaku kuhusu
maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.
Ujumbe huo umeongozwa na kiongozi wa ujumbe huo Dkt. Tim Kelly, wakiambatana na Mratibu wa
Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, Bw. Honest Njau pamoja na watumishi wanaotumika
chini ya mradi huo.
Lengo la ugeni huo ni kukagua maendeleo ya
utekelezaji wa maeneo yaliyoainishwa kwenye mradi huo ambapo walifanikiwa
kutembelea Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) na kupokea taarifa ya maendeleo ya utengenezaji wa
mifumo ya tehama inayotengenezwa kupitia mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amezungumzia mifumo mitatu ya
tehama inayotengenezwa kupitia mradi huo ambayo itarahisisha upimaji kazi wa
watumishi na taasisi pamoja na kumsaidia mwananchi kuzifahamu taasisi za
Serikali na taarifa zake kuhusu huduma zinazotolewa.
Aidha,
ameitaja mifumo hiyo kuwa ni mfumo wa upimaji kazi wa watumishi (PEPMIS) mfumo
wa upimaji kazi kitaasisi (EPIPMIS) na mfumo wa daftari la huduma za Serikali
na taarifa zake (Government Servises Directory).
Bw. Daudi amesema
kuwa lengo la kutengeneza mifumo hiyo ni Serikali kuboresha utoaji wa huduma
kwa wananchi kwa urahisi kupitia mifumo ya kisasa ya tehama na kutimiza dhamira
ya Serikali ya kuwa na Tanzania ya Kidijitali.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba amesema kuwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali mamlaka hiyo itafikisha mawasiliano ya mtandao wa Serikali kwenye wilaya na halmashauri zote nchini ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Sambamba na hilo amezungumzia maeneo mengine yanayotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na maboresho ya miundombinu ya kuhifadhi mifumo katika sehemu za kuhifadhi mifumo pamoja na kuongeza uwezo wa matumizi ya intaneti yenye kasi katika taasisi zote za umma
Amesema kuwa lengo la mradi ni kuboresha huduma za mtandao kwa urahisi na kuwezesha upatikanaji wa huduma za kiuchumi kwa njia ya mtandao kama vile mawasiliano baina ya wafanyabiashara (wauzaji na wanunuzi)
Akiongea kwa niaba ya ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia, Dkt. Tim Kelly, Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Dunia wa Mradi wa Kidijitali Tanzania amesema ziara ya ujumbe huo imelenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika maeneo yote ya utekelezaji toka ulipoanza kutekelezwa mwezi wa Septemba, 2021.
Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Honest Njau akizungumza wakati ujumbe wa Benki ya Dunia wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali walipotembelea Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Xavier Daudi
Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Honest Njau (kushoto) akizungumza na Bw. Xavier Daudi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Dunia Dkt. Tim Kelly wakati ujumbe wa Benki ya Dunia wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali walipotembelea na kufanya mazungumzo na watendaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Honest Njau (kushoto) akiteta jambo na Bw. Xavier Daudi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora baada ya Ujumbe wa Benki ya Dunia wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kutembelea na kufanya mazungumzo na watendaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba (kushoto) akiteta jambo na Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, Bw. Honest Njau wakati Ujumbe wa Benki ya Dunia ulipotembelea na kufanya mazungumzo na na Mamlaka hiyo katika ofisi zake zilizopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ziara ya Ujumbe wa Benki ya Dunia katika ofisi za Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mamlaka ya Serikali Mtandao zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kutembelea na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Tanzania ya Kidijitali
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari.
No comments:
Post a Comment