Habari za Punde

Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Afunga Kongamano la Pili la Mtandao Elimu Tanzania

Waziri wa E,imu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa akizungumza wakati akifunga Kongamano la Pili la Mtandao wa Elimu Tanzania,lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwali Nyerere Jijini Dar es Salaam na Kuwashirikisha Wadau mbalimbali wa Elimu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibaer Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema kuwepo kwa mageuzi katika sekta ya elimu kutaweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa Tanzania.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua kongamano la pili la mtandao wa  elimu Tanzania lililowashorikisha wadau  wa sekta ya elimu katika  ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salamu.

Amesema Serikali kwa sasa Iko katika hatua ya mwisho ya kukusanya maoni kwenye sera ya elimu Ili ije kupitishwa na bunge Mara baada ya kukusanywa kwa maoni na  Watalaamu watafiti katika sekta hiyo.

Aidha  ameleza kuwa nchi nyingi  dunia hivi sasa zimekuwa mstari wa mbele katika kupigania mageuzi katika  mfumo wa elimu.

Mkutano huo wa Wadau wa sekta ya elimu umelenga pia kujadili uwekezaji Katika miundombinu ikiwemo majengo,Ajira za walimu pamoja na stahiki zao.

Serikali kupitia kikao hiki inasubiri maoni ya wadau kuja na elimu inayoendana na mazingira halisi ya mtanzania Ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.