Habari za Punde

WFP Yakabidhi Vifaa vya Mawasiliano kwa Ofisi ya Waziri Mkuu

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akifafanua jambo wakati wa Makabidhiano ya vifaa hivyo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (kushoto) akipokea Kompyuta mpakato kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gibson (kulia) ikiwa ni ishara ya kupokea vifaa hivyo.

                              (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi wetu-Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga amepokea vifaa vya mawasiliano vitakavyotumika katika kukabiliana na maafa mbalimbali hapa nchini ambavyo ni  Ndege zisizo na Rubani (Drones) vyenye thamani ya shilingi Milioni 102,741,400 vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma Mhe. Ummy  alisema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu  kutekeleza shughuli za uratibu na  udhibiti  wa maafa  mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa  katika picha ili kupata  majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.

Mhe. Ummy alieleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali  na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.

 “Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP  binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”Alisema Mhe. Ummy.

Aidha aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu alibainisha kwamba  Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na  (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.

 “Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukuwa mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa uraisi”.

Aidha  Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gibson alifafanua kuwa mradi huo  ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na viupembeel vya serikali na kuwekeza katika kilimo, elimu, maafa pamoja na wakimbizi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.