Habari za Punde

Yanga SC Yaendeleza Ubabe kwa Kuinyuka Coastal Union kwa Bao 2-0, Mayele na Morrison Watupia.

 

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU yaYanga imeendelea kutoa dozi  kwenye ligi ya NBC mara baada ya hii leo kuichapa  timu  ya Coastal  Union kwa mabao 2-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.

Ni Mayele tena ambaye aliingia kipindi cha pili na kupachika bao la pili kwenye mchezo huo akipoke pasi ya kichwa kutoka kwa mkongo beki kisiki mwenzake Shaban Djuma na kuzamisha moja kwa moja  nyavuni.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Benard Morrison kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka Jesus Moloko ambaye pia aliumia kwenye mchezo huo na kulazimishwa kutoka baada ya kuchezew rafu mbaya na mlinzi wa Coasta Union

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.