Habari za Punde

DC Moyo Awataka Walimu Kuacha Kuwafanyia Ukatili wa Kijinsia Wanafunzi

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akizundua kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa
Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo wakati wa uzizunduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa
Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo wakati wa uzizunduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewataka walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wanaowafundisha ili taifa liweze kupata wasomi wengi ambao wanauwezo wa kuja kukisaidia Taifa hapo baadae.


Akizungumza wakati wa kuzindua vitabu vyenye muongozo wa waziri mkuu namna ya kuwapata viongozi katika njia sahihi ambayo haitakuwa na ubabaishaji, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa Kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakiaribu taswira halisi ya kada ya ualimu.

 Moyo alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya walimu kufanya mapenzi na wanafunzi na kuwafanyia ukatili wanafunzi kwa makusudi hivyo walimu wanapaswa kutoa taarifa kwa mwalimu yeyeto atakayekutwa anafanya vitendo vya ukatili.

 

Alisema kuwa kazi kubwa ya mwalimu ni kuwafundisha wanafunzi waweze kufaulu na sio kuwafanyia ukatili wanafunzi.

Lakini pia mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa vitabu vya muongozo vinataka wateuliwa wateuliwe kwa kufuata misingi sahihi na sio kwa njia ya rushwa au kujuana.

 

Moyo alisema kuwa muongozo huo utumike vile ambavyo unastahili kulingana na maagizo ya waziri mkuu Kassim Majaliwa yanayotaka kuwa na yawe hivyo hivyo.

 

Aidha Moyo alimazia kwa kusema kuwa walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa wanafanya vizuri kwenye kufundisha wanafunzi ndio maana matokeo yake yamaekuwa mazuri mwaka hadi mwaka.

 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa walimu wanafanya kazi kubwa kuwafaulisha wanafunzi licha ya kuwa wanakabiriwa na changamoto mbalimbali hasa mazingira wanayofanyia kazi.

 

Ngwada alisema kuwa Halmashauri inatamani kumaliza changamoto zote za walimu hasa kuboresha miundombini ya kufundishia na mazingira wanayoishi lakini kikwazo kikubwa kwao ni ufinyu wa bajeti ambayo wanayo.

 

Alisema kuwa wakifanikiwa kupata bajeti basi watakuwa wanatatua changamoto kadili wanavyoweza ili kuwasaidia walimu kufundisha katika mazingira mazuri.


Awali akisoma muongozo huo kwa mkuu wa wilaya ya Iringa,kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Gerald Mwamuhamila alisema kuwa kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kina toa utaratibu wa Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa.

 

Mwamuhamila alisema kuwa Viongozi wa Elimu ni nguzo muhimu katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.

Hivyo Uteuzi wa Viongozi hawa hupaswa kufanywa kwa Umakini Mkubwa kabla ya kuwakabidhi dhamana ya Kuongoza. 


Alisema kuwa Mwongozo huo umeunda kamati zitakazoshughulikia na Uteuzi wa Viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi ngazi ya Mkoa. Kabla ya Mwongozo huu Viongozi wa Elimu walipendekezwa na Kuteuliwa na kamati ya watu wachache Tofauti na itakavyokuwa sasa. 

Mwamuhamila alipongeza kuwa Mwongozo Umebainisha Sifa za Kimuundo na Sifa za utendaji wa Kila Cheo cha Uteuzi.


Aidha kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa kitabu cha Mkakati wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji ngazi ya Elimumsingi kimefafanua jinsi ya kuboresha Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kuweka Mikakati thabiti yenye kutekelezeka. Kitabu hiki kimetoa hali ya Elimumsingi Nchini, Mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimumsingi, Usimamizi,ufuatiliaji na tathmini ya mikakati, Ushiriki wa  wadau katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati.

 

Kitabu cha tatu utakacho kizindua leo ni kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimumsingi na Kitabu hicho kimebainisha Changamoto, hatua za kuchukua ili kukabiliana na changamoto hizo, pamoja na kubainisha kinachotakiwa kufanyika ili kushirikisha wasimamizi wa Elimu, Wazaz/Jamii, Viongozi na wadau mbalimbali kuhusu usimamizi madhubuti wa Elimu ya Awali, Msingi na  Sekondari.

Lakini pia hatua zilizobainishwa zinakusudiwa kutumiwa kama mwongozo kwa Viongozi katika ngazi zote Taifa, Mkoa, Halmashauri, Kata, Kijiji,Mtaa na Shule katika utatuzi wa changamoto zinazokwamishaufundishaji na ujifunzaji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.