Habari za Punde

Dkt. Abbasi Ataka Wazalishaji wa Maudhui kuzingatia Maadili

 

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati akifungua Warsha ya Uhamasishaji wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maudhui bora ya Ndani, uliofanyika  Jijini Dar es Salaam  ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Washiriki wa Warsha ya Uhamasishaji wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maudhui bora ya Ndani, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi, akifungua warsha hiyo.iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Na Shamimu Nyaki

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amefunga Warsha ya Uhamasishaji wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maudhui bora ya Ndani, leo Septemba 16,2022 Jijini Dar es Salaam  ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Dkt. Abbasi  amefunga Warsha hiyo kwa Niaba ya Waziri wa wizara hiyo Mhe.Mohamed Mchengerwa, ambapo amesisitiza  Waandaaji wa Maudhui kuzingatia Mila, Desturi, Utamaduni na matumzi sahihi ya Lugha ya kiswahili katika Maudhui hayo.

"Wizara inaendelea kusisitiza uzalishaji wa Maudhui bora yanayozingatia Mila na Desturi za Tanzania katika eneo la Sanaa na Utamaduni kwakua ndio utambulisho wa Taifa letu"

Katibu Mkuu Abbasi amewataka wadau wa Maudhui  kutanguliza  ajenda za kitaifa wanapokua wanazalisha na kutangaza maudhui kwa walaji.

Amesisitiza matumizi ya maneno yenye staha na kuepuka dhihaka hasa katika Maudhui ya Mitandaoni ambayo jamii haifurahishwi nayo, huku akisisitiza hakuna uhuru bila mipaka.

Aidha, ameahidi wizara yake itashirikiana na TCRA katika maazimio yote yaliyofikiwa katika Warsha hiyo, na ipo tayari kutoa ushirikiano katika maeneo ya utoaji wa Tuzo kwa Wazalishaji Bora wa Maudhui kwakua imefanikiwa katika eneo la  kuandaa Tuzo za filamu na Muziki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabir Bakari amesema Warsha hiyo imetoa maoni na mapendekezo bora katika kuzalisha na kusambaza Maudhui ya ndani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.