STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 09 Septemba,2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali
Mwinyi amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani iliopo ili Serikali iweze kufikia malengo ya kuwaletea
maendeleo.
Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo katika
salamu alizotoa kwa waumin walioshiriki Ibada ya sala ya ijumaa iliofanyika
Masjid Lutta, Kiembesamaki Mkoa Mjini Magharibi.
Amesema hivi sasa nchi ina amani ya
kutosha, hivyo ni wajibu wa wananchi kuendeleea kudumisha hali hiyo, ili kutoa
fursa kwa Serikali kutekelza malengo yake ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, aliwataka wananchi popote pale
walipo kufanya juhudi kutimiza wajibu
wao ili waweze kupata mafanikio.
Nae, Katibu wa Mufti wa Zanzibar
Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwaomba waumini kumuombea Dua Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi ili amfanyie wepesi
katika kutekeleza malengo yake ya kuiletea nchi maendeleo.
Mapema, Khatibu katika sala hiyo ya
Ijumaa Sheikh Said Khalfan Said aliwataka waumini kurudi kwa Mwenyezi Mungu na
kutekeleza maamrisho yake pamoja na kumshukuru kwa neema ziliopo.
Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment