Habari za Punde

Rais DK Hussein Mwinyi aelekea Dar kuhudhuria Kikao cha Kamati Kuu ya CCM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi   wakati akiagana na Viongozi wa Vyomo vya Ulinzi na Usalama alipokuwa akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo kesho atahudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM,kitakachofanyika ukumbi wa Ofisi ya CCM Lumumba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto)  alipokuwa akiagana  na Makamo wa Pili wa Rais Zanziar Mhe.Hemedi Suleiman leo alipoondoka  kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo atahudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM,kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Lumumba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na  Mkewe Mama Mariam Mwinyi alipokuwa akisalimiana na Viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makala (katikati) wakati wa mapokezi yake mara alipowasili   katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam leo,  akihudhuria katika Kikao cha Kamati Kuu kitachofanyika kesho katika  Ofisi ya CCM Lumumba.
[Picha na Ikulu.] 06 sept 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.