Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ashiriki Maziko ya Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar Marehemu John Ramadhan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa heshima ya mwisho kwa Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar, wakati wa Ibada ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi alishirki katika mazishi ya Askofu Mkuu mstaafuJohn Aukland Ramadhan yaliofanyika Kanisa la Anglican Mkunazini, Mkoa Mjini Magharibi.

Katika hafla hiyo, iliohudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa kitaifa, wakiwemo Mawaziri kutoka SMZ na SMT, Waziri wa Nchi (OMPR) Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma alitoa salamu za rambirambi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema wakati wa uhai wake Hayati Askofu John Ramadhan alitoa mchango mkubwa katika kuleta ustawi wa Taifa.

Alisema Hayati Askofu Ramadhan alishirikiana kikamilifu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Viongozi mbali mbali katika kuhimiza na kusimamia amani nchini.

Waziri Hamza alisema ana matumaini makubwa kuwa Kanisa litayaendeleza yale yote aliyoyaasisi na akatumia fursa hiyo kutoa mkono wa pole kwa familia na Kanisa Anglican kwa ujumla.

Hayati Askofu Mkuu mstaafu John Ramadhan, mwenye umri wa miaka 90,  alifariki dunia Septemba 12, 2022 katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili alikokuwa amelezwa kwa vipindi tofauti.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.