Habari za Punde

Dkt.Jingu Amekutana na Kuzungumza na Timu ya Wataalamu wa CIMA Research Foundation

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizugumza  wakati wa kikao  alipokutana na timu ya Wataalam wa CIMA Research Foundation wanaorasimisha mfumo wa MYDEWETRA kwa ajili ya tahadhari ya  mapema  kabla ya maafa kutokea kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi hiyo  Oktoba 06, 2022 Jijini Dodoma.
Mtafiti kutoka  Taasisi ya CIMA Foundation Bi. Anna Mapelli akieleza jambo  wakati wa kikao hicho.
Mtafiti wa Taasisi ya CIMA Foundation Bw. Antonio Libroia akiwasilisha hoja kuhusu utekelezaji wa mfumo wa MYDEWETRA kwa ajili ya tahadhari ya mapema walipokutana Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma

Baadhi ya Wajumbe  wakifuatilia kikao cha kupokea taarifa ya Wataalam wa CIMA Research Foundation wanaorasimisha mfumo wa MYDEWETRA kwa ajili ya tahadhari ya  mapema walipokutana Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma Oktoba 06, 2022.

               (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.