Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga
ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mradi mradi wa kujenga
uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi kupitia
Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya
Tabianchi Katika Mipango ya Nchi.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa
Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Septemba 30, 2022 kimehusisha wajumbe
kutoka Wizara za kisekta, sekta binafsi na Asasi
za Kiraia
Lengo la mradi huo ni
kuimarisha uwezo wa nchi katika kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kwa
kujumuisha, masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika mipango ya maendeleo.
Mradi utawezesha
wizara na taasisi kuwa na mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na
kuimarisha uratibu wa taasisi na wadau husika katika kutekeleza mipango ya
uhimilivu na maendeleo ili kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka katika sekta
zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, matokeo
tarajiwa ya utekelezaji wa mradi yanatarajiwa kuwa ni kuboresha uwezo wa
kitaifa wa upangaji wa mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuimarika
kwa uratibu wa taasisi na wadau.
Pia kuimarisha ukusanyaji wa takwimu kutoka
katika sekta zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi pamoja na Mpango
wa Taifa wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kuandaliwa na kupitishwa.
Afisa
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Asia Akule akiwasilisha Mradi mradi wa
kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi
kupitia Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya Kuhimili Athari za
Mabadiliko ya Tabianchi Katika Mipango ya Nchi kilichofanyika leo Septemba 30,
2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya
Kitaifa ya Mradi mradi wa kujenga uwezo wa utayari wa nchi kuhimili athari za
Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Kuandaa Mpango wa Taifa wa Kuhuisha Masuala ya
Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Katika Mipango ya Nchi mara baada ya
kufanyika kikao hicho leo Septemba 30, 2022 jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment