Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Patricia Leverley kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma
Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato Mkoani humo 
Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato Mkoani humo tarehe 30 Oktoba, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.