Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aondoka Nchini Akielekea Nchini Uganda Kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Nchi hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na  Viongozi mbalimbali wa Serikali  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchi Uganda leo 8-10-2022, kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimia na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Uganda kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.