Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar leo (30/09/2020) wamebariki kuruhusiwa Michezo ya Ngumi kupitia hoja iliyotolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita.
Wakichangia hoja hiyo, katika kikao cha Baraza huko Chukwani, wajumbe hao waliipongeza Wizara inayoshughulikia michezo kwa kulisimamia jambo hilo ambalo limewahi kuwasilishwa katika vikao vya Baraza lilivyopita.
Akiwasilisha hoja hiyo Mhe. Tabia alisema mijadala mbali mbali imeendeshwa kwenye vikao vya wadau wa michezo, vyombo vya habari na hata wananchi walithubutu kwenda kwenye Baraza la Taifa la Michezo kudai kuwepo kwa mchezo huo.
Aliongeza kuwa, katika kikao cha Baraza la Wawakilishi cha mwaka 2021, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamo wa Pili wa Rais ambae ndio Kiongozi wa Serikali ndani ya Baraza la Wawakilishi aliliahidi Baraza la Wawakilishi kuwa Serikali itakusanya maoni ya wananchi juu ya michezo hiyo ili baadae taarifa ya maoni hayo iwasilishwe kwenye kikao cha Baraza hilo.
No comments:
Post a Comment