Na Oscar Assenga,TANGATIMU ya Mchezo wa Riadhaa ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeng’ara katika Mashindano ya Shimiwi yanayoendelea Jijini Tanga huku wakimbiaji wake kuchukua nafasi za kwanza na pili katika mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tanga Ufundi.
Wachezaji wa timu ya Elimu ilianza kwa kasi katika mchezo huo wa Riadhaa ambapo wakimbiaji wake walikuwa hari kubwa ya kukimbiza upepo ili kuweza kupata ushindi katika mashindano hayo.
Katika mchezo huo timu ya wanaume imefanya vizuri kwa upande wa mita 100 kupokezana vijiti huku kwenye zile za mita 200 wakiibuka washindi wa pili.
Kwa upande wa michezo mengine timu za Wizara hiyo walipambana mpaka kufikia hatua ya nane bora kwa mchezo wa kuvuta kamba ,mpira wa miguu,mpira wa pete .
Wakimbia Anitha Kihiyo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alishika nafasi ya pili nakikimbia mita 100 na Martine Zulumo akichukua nafasi ya pili imekwenda Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na hivyo ametwaa media ya dhahabu.
Kwa upande wa riadhaa kupokeza vijiti wanaume nafasi ya kwanza imeenda kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Akizungumza kuhusu mashindano hayo Makamu Mwenyekiti ywa timu ya Elimu Sports Deogratius Wenga alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa na ushindani mkubwa.
KAMATI YA KUSIMAMIA MADALALI WA MABARAZA YA ARDHI YAKAGUA KAMPUNI ZA
UDALALI DSM
-
Na Munir Shemweta, WANMM
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza
ya Ardhi nchini ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Ku...
6 hours ago
No comments:
Post a Comment