IMEELEZWA kwamba zipo fursa nyingi za kiuchumi na uwekezaji zinazoweza kutumika kwa ushirikiano na kuchangia kuleta maendeleo makubwa kati ya Zanzibar na nchi za Falme za Kiarabu (UAE).
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ameyasema hayo Ofisini
kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na
kuzungunza na Balozi Mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu Bw. `Saleh
Alhemeiri kuhusiana na ushirikiano katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi na
kijamii.
Mhe. Othman
amesema kwamba nchi kwa kuwa zinao uhusiano mkubwa wa kijamii hivyo fursa za
mashirikiano katika maeneo ya uchumi, wa bluu , utamaduni, uvuvi, Kilimo na
biashara katika sekta ya huduma ya usafiri wa Anga.
Amefahamisha
kwamba Zanzibar inaweza kuutumia na kufaidika na uzoefu mkubwa uliopo katika
nchi hizo ili kusaidia pamoja na mambo
mengine kujenga uwezo wa Zanzibar katika maeneo mbali mbali kwenye sekta hizo na kuweza kuwa na tijha
kubwa kimaendeleo.
Ameongeza
kwamba sekta ya uchukuzi wa anga hivi sasa inamuelekeo wa kuwa sekta kubwa na
tegemeo muhimu la kiuchumi inayoweza kusaidia Zanzibar kuweza kupiga hatua
kimaendeleo.
Naye Balozi
Mdogo wa UAE Bw. `Saleh Alhemeiri, asmesema kwamba UAE ipo tayari kuisaidia Zanzibar katika maeneo mbali
mbali ya sekta hizo ili kuendelea kujenga uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya
nchi hizo mbili.
Amesema
kwamba nchi hiyo wanaweza kusaidia pia kutoa mafunzo kwa vijana kutoka Zanzibar
ili kuisaidia Zanzibar kuwa kituo muhimu katika sekta ya huduma ya usafiri wa
Anga.
Wakati huo
huo Mhe. Othman amekutana na ujumbe Watendaji wa Taasisi kutoka Ofisi ya Rais
ya Ufuatiliaji ,usimamizi wa Utendaji Serikalini na kuwaeleza kwamba taasisi
hiyo inakazi kubwa ya kusaidia kunyanyua na kutimiza matumaini ya wananchi hasa
wanyonge kwa kuwepo na kuimarika utolewaji
wa huduma za kijamii kama matarajio ya wananchi yalivyo.
Mhe. Makamu
amesema kwamba Taaisi hiyo ni nyenzo muhimu katika kufikia matarajio ya kweli
na matumaini mazuri ya wananchi iwapo watendaji hao wataangalia, kuanisha na
kuyafanyia kazi maeneo mbali mbali muhimu yatakayosaidia kunyanyua uchumi na
maendeleo ya Z anzibar.
Amefahamisha
kwamba yapo maeneo mengi yanayohitaji kufanyiwa kazi ili kusaidia ipasavyo nchi katika kunyanyua matumaini na matarajio
ya wananchi wa Zanzibar hasa kwenye kufikia upatikanaji wa huduma bora za
kijamii na maendeleo kwa jumla.
Naye Kiongozi
wa ujumbe huo ambaye ni naibu mtendaji
Mkuu wa Taaisi hizi Ndugu Josphine Kimaro amesema kwamba taasisi hiyo imeundwa
katika kusaidia utekelezaji wenye tija kwa maeneo ya vipaumbele vya maendeleo
vilivyowekwa na serikali ikiwemo uchumi wa bluu, miundombinu,huduma za jamii
kama afya , umeme na maji sambamba na
kuwafahamisha wananchi kuhudu juhudi za serikali kwenye hatua za utekelezaji wa
mambo mbali mbali yalivyopfikiwa.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha
Habari leo tarehe 18.01.2023.
No comments:
Post a Comment