Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Mcheza Filamu Maarufu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (IFAD), Davos, Uswizi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani Idris Elba ambaye ni Balozi wa Hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD pamoja na Mke wake Sabrina Elba walipokuwa Davos nchini Uswizi. 

Mfanyabiashara mkubwa na Mwenyekiti mwenza wa Timu ya Manchester United ya Uingereza Avie Glazer akisikiliza kwa makini wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiitangaza Tanzania katika mkutano uliofanyika Davos, nchini Uswizi. 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa Kuitangaza Tanzania katika Sekta ya Uwekezaji kwenye ukumbi wa Mikutano wa Congress, Davos nchini Uswizi tarehe 19 Januari, 2023. Wa kwanza kushoto aliyevaa miwani ni mfanyabiashara mkubwa na Mwenyekiti mwenza wa Timu ya Manchester United ya Uingereza Avie Glazer akisikiliza kwa makini wakati Mhe. Rais alipokuwa akiitangaza Tanzania.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.