Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali afungua kongamano la miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Muhammed Mussa akifungua kongamano la miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, lililoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KISTSO), hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt.Idrisa Muslim Hijja, Mbweni Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi (KISTSO) Hassan Songoro Maulid akizungumza katika kongamano la miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, lililoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KISTSO), hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt.Idrisa Muslim Hijja, Mbweni Zanzibar.

PICHA NA MARYAM KIDIKO – KIST.

Na Issa Mzee - KIST..

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Muhammed Mussa, amesema ipo haja kwa kila Kijana kuelewa dhana nzima ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ili waweze kujuwa namna ambavyo Zanzibar inapiga hatua katika maendeleo.

Alisema hayo wakati akifungua kongamano la miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, lililoandaliwa na Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KISTSO), lililofanyika katika Ukumbi wa Dkt.Idrisa Muslim Hijja, Mbweni Zanzibar.

Waziri Lela ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo amesema harakati mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Afya, Maji na Elimu ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, hivyo ipo haja kwa kila kijana kufahamu umuhimu na faida za Mapinduzi ya Zanzibar.

Alieleza kuwa, ikiwa vijana watapata  ufahamu wa kina kuhusu umuhimu wa Mapinduzi  wataweza kujuwa faida ya kuwa na Umoja, Mshikamano na Upendo  kama waliokuwa nao wanamapinduzi wa Zanzibar.

Aidha alitumia fursa hiyo, kuupongeza uongozi wa Taasisi ya Karume pamoja na Serikali ya wanafunzi ya Taasisi hiyo, kwa kuanzisha kongamano hilo ambalo linaifanya Taasisi ya Karume kuwa ni Chuo cha kwanza Zanzibar kuanzisha kongamano la Mapinduzi.

Katika kongamano hilo, mada mbalimbali ziliweza kuwasilishwa ikiwemo,Historia ya ukombozi wa Zanzibar, historia ya Taasisi ya Karume, Sera ya Elimu ya ufundi, pamoja na Mafanikio ya miaka miwili ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.