Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aufungua rasmin Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wafadhili waliojenga Msikiti wa Kilimani Masjid Fatma Ahmad Merdas, alipowasili katika viwanja vya Msikiti huo kwa ajili ya kuufungua na kujumuika na Wananchi kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma Ahmad Merdas baada ya kuufungua rasmin leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuufungua rasmin Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-2-2023, na kujumuika na Wananchi katika Ibada ya Sala ya Ijumaa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Bw.Ahmed Baker na Bw. Ali Albwardy,Wafadhili wa ujenzi wa Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kuufungua na kujumuika na Wananchi katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika baada ya ufunguzi wa Msikiti huo, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Sheria, Katiba,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kuufungua rasmin Msikiti wa Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja, uliyofanyika leo 10-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza hutuba ya Ibada ya Sala ya Ijumaa akisoma na Hatibu Sheikh. Abdallah Zuberi Maruzuku, kabla ya Sala, iliyofanyika katika Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj.Dkt. Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Mfadhili wa Masjid Fatma Ahmad Merdas Bw.Ali Albwardy na Naibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Fatma Ahmad Merdas Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja uliofunguliwa leo 10-2-2023 kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.