Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ni wajibu kwa viongozi wa ngazi mbali
kuwa karibu na wananchi katika kusaidia kujenga umoja na ushirikiano miongoni
mwao hasa katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makau Mwenyekiti wa ACT
Wazalendo upande wa Zanzibar, ameyasema hayo huko viwanja vya Kwabimtoro mjini
Unguja baada ya kukamilisha siku ya kwanza ya ziara yake ya kutembelea wagonjwa
na vizuka katika majimbo mbali mbali ya
Uguja na Pemba.
Aidha Mhe. Othman amesema pia
pamoja na mambo mengine ziara kama hizo ni muhimu kwani zinasaidia sana
viongozi kupata funzo kubwa la kufahamu hali na maisha ya watu yalivyo na
kutafakari juu ya namna bora ya kuendeleza umoja.
Mhe. Othman paia amesema kwamba
ziara hizo pia zinatoa nafasi kwa viongozi kusikiliza moja kwa maoja matatizo
ya wananchi na kuweza kufahamu hivyo kuwezesha
kutafakari namna ya kutafuta mbinu za pamoja za kuyatatu.
Mhe Makamu amewataka wale weto
waliopatwa na mtihani wa maradhi ya aina mbali mbali kuendelea kuwa na subra na
kufahamu kwamba maradhi ni mtihgani kutoka kwa mola muumba ambayo hupewa
wanaadamu ili wapate kumkumbuka mola wao.
Aidha ameahidi wale wote
aliowatembelea kwamba serikali kupitia viongozi mbali mbali wapo pamoja nao
katika kusaidina kutafuta tiba ya maradhi yao.
Mapema Katibu wa Haki za Binaadamu
na Makundi Maalum wa ACT – Wazalendo Pavu Abdalla Juma, amesema ziara hizo ni
muondelezo wa urithi muhimu kutoka kwa mtangulizi wa Mhe, Makamu Marehemu maalim Seif Shariff
Hamad amabazo alizifanya kila ifikapo mwezi wa ramadhani na zinasaidia sana
katika kujenga umoja na mshikamanoo miongoni mwa wananchi na viongozi wao.
Naye Katibu wa ACT- Wazalendo Mkoa
wa Mjini Magharib Mahamoudu Ali Mahinda, amasema kwamba chama hicho katika
ngazi ya Mkoa wa Mjini kimeanzisha mfuko maalum wa faraja kwa ajili ya kusaidia wenye
shida na changamoto mbali mbali ambao utakua na mwendelezo wa ziara za
kutembelea wagonjwa na wenye shida mbali mbali.
Nao wagonjwa mbali mbali
waliotembewa wamemshukuru Mhe. Othman
kwa uamuzi wake huo na kusema kwamba mwendelezo wa ziara kama hizo
zinaofanywa hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani zinasaidia sana
kujenga umoja na pia kuongeza imani kati viongozi na wananchi wao.
Mhe. Othman katika ziara hiyo ametembelea
majimbo Chumbuni, Shaurimoyo, Amani , Magomeni , Kwahani, Mpandae, Jang’ombe,
Kiwajuni na Malindi katika wilaya ya mjini Unguja ambapo kesho anatarajia kutembelea
majimbo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe 26, 03,2023.
No comments:
Post a Comment