Habari za Punde

SMZ Itaendelea Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa

Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuwaenzi na kuwakumbuka Viongozi wa Kitaifa ambao ni Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kupigania uhuru, kusimamia na kuongaza nchi baada ya Mapinduzi Matukufu .

Akiyasema hayo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mheshimiwa Simai Mohamed Said  huko Migombani Wilaya ya Mjini, wakati wa ziara ya kusoma dua katika kaburi la Marehemu  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi .

Amesema kuwa Kiongozi huyo wa Awamu ya Pili alifanya mengi makubwa  kwa wananchi wa Zanzibar ya kuiyongoza nchi na kuisimamia baada ya Mapinduzi  Matukufu ya Zanzibar  na hadi sasa matunda yake yanaonekana

Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al- hajj , Dk. Hussein Mwinyi kwa kutambua mchango wake mkubwa  alioutoa kwa Wananchi wa Zanzibar Rais wa Awamu ya Pili  Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi,  Mwenyezi Mungu amlaze Mahala Pema peponi.

Aidha alisema kuwa  mambo mengi mazuri aliyoyafanya katika nchi hii wakati wa uongozi wake hadi sasa tunajivunia na kuahidi kuyatunza, na kuyaenzi  kwa kizazi kijacho  .

Alifahamisha kuwa Rais Mstaafu atakubukwa sana katika  Kuitetea Katiba ya Zanzibar ambayo ilisaidia kuzaliwa Baraza la Wawakilishi na kuiahidi familia hiyo kuwa pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hali na mali

Nae Mkuu wa Familia Mustafa Aboud Jumbe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia hiyo  kwa kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ujio huo wa kufanya ziara ya kusoma dua kwa Marehemu Mzee wao mbae amelala katika eneo hilo tangu 2016 pamoja na ndugu  zao waliozikwa katika eneo hilo.

Amesema kuwa amefarajika na ujio huo na kumuomba Mwenyezi Mungu awasaidie viongozi walikuwepo madarakani  kuingoza nchi katika hali ya salama na Amani

Ibada ya kumuombea dua  Rais wa Awamu ya Pili  Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, imeongozwa na Sheikh Sharifu Abrahmani kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar

Kila ifikapo Aprili  mosi hadi saba ya kila Mwaka ni wiki ya Maadhimisho ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.