Habari za Punde

Nyota wa Zamani wa Zanzibar Heroes na Taifa Stars Mohammed Kachumbari Amefariki Dunia Leo Jijini Dar es Salaam

Aliyekuwa  beki wa zamani wa Timu ya Kikwajuni, Small Simba, Mlandege na kumalizia Timu ya Mafunzo Zanzibar Mohammed Kachumbari amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirisha leo kwa boti ya mchana kutika Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Zanzibar baada kuwasili kwa mwili wa marehemu.

Marehemu Kachumbari aliwahi kuchezaa Timu za Taifa ya Zanzibar na Tanzania na kuwa Kocha wa Timu ya Mafunzo Zanzibar.

Inallilah Waina Iilah Rajiun.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.