Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Ndg. Mohammed Raza Hassanali

 


Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimepokea kwa masikitiko na huzuni mkubwa taarifa ya kifo cha Kada,Mwanasiasa na Mfanyabiashara maarufu Ndugu Mohamed Raza Hassanali aliyefariki leo Juni 08,mwaka 2023 katika Hospitali ya Aghacan Jijini Dar es saalam.

Ndugu Mohamed Raza,amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za ndani ya Chama na Serikali ambazo ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja na Mshauri wa Rais wa Zanzibar awamu ya tano katika masuala ya Michezo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki,Wana CCM na Watanzania wote walioguswa na msiba huo amewasihi waendelee kuwa na subira katika kipindi chote cha msiba huo.

“Enzi za uhai wake  Mohamed Raza alikuwa ni kiongozi aliyelinda na kukipigania Chama chetu na alikuwa ni kada muadilifu,mchapakazi na mzalendo  mwenye maono ya kimaendeleo ndani ya Chama na Serikalini”, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi.

Ndugu Raza, alizaliwa Julai 08,1962 katika Mtaa wa Mkunazini Unguja, hadi anafariki alikuwa ni Kada wa CCM na Mfanyabiashara anatarajiwa kuzikwa leo saa 11:00 jioni Juni 08,mwaka 2023 katika Makaburi ya Kisutu Dar es saalam.

             Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI” 

KHAMIS MBETO KHAMIS

1 comment:

 1. Makamu wa Rais wa Zanzibar, Usman Masood na Maulana Rajani walihudhuria mazishi ya mwanasiasa wa Zanzibar, Tanzania, katika nchi ya Afrika Mashariki, Muhammad Raza, usiku wa kuamkia leo.

  Zanzibar, Juni 9: Makamu wa Rais wa Zanzibar, Usman Masood na viongozi wengi wa kisiasa wa Zanzibar na Dar es Salaam mbali na Waafrika-Wahindi walihudhuria mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Uzini, Muhammad Raza, kiongozi wa kisiasa wa Khwaja Shia mwenye asili ya Kihindi kisiwani Zanzibar nchini Tanzania. , Afrika Mashariki Mbali na wasomi wa Kisunni wa Shia, Maulana Hasan Ali Rajani, rais wa Ligi ya Kitaifa ya India ya Kerala, chama cha kisiasa cha India, Mkoa wa Gujarat, alikuwa na ushiriki maalum. Viongozi wa kisiasa na kijamii wa nchi hiyo akiwemo Rais wa nchi hiyo Samia Hassan Sulawhi na makamu wa rais pia walifika kutembelea.Maulana Rajani Hassan Ali kutoka Dar es Salaam alielezea masikitiko yake na kusema kwamba huduma za marehemu Muhammad Raza kwa kurejesha demokrasia. haki za binadamu hazisahauliki Na kifo chake kina madhara makubwa sana kwa shirika la haki za binadamu. Mwishowe Maulana Rajani alimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusema, “Ewe Mola mpe nafasi marehemu huyu katika rehema zake, na uwape subira waliofiwa. Akitoa salamu zake za rambirambi na pole kwa wafiwa na wanafamilia, Rajani alisema katika kipindi hiki cha majonzi pia tunashiriki majonzi yao.

  From Hasan Bhai. East Africa Tanznia Dar Es Salaam Cell No +255745344366 whatsaap +919998269850


  The Vice President of Zanzibar, Usman Masood, and Maulana Rajani were present at the late night funeral of the political figure of Zanzibar, Tanzania, in the East African country, Muhammad Raza.

  Zanzibar, June 9: Zanzibar's Vice President Usman Masood and many Zanzibar and Dar es Salaam political figures besides Indian-Africans attended the funeral of former MP for Uzini, Muhammad Raza, an Indian-origin Khwaja Shia political leader on the island of Zanzibar in Tanzania , East Africa. In addition to Shia Sunni scholars, Maulana Hasan Ali Rajani, president of the Indian National League of Kerala, India's political party, Gujarat Province, had a special participation. was The country's political and social personalities, including the country's President Samia Hassan Sulawhi, and the vice president also came to visit. Maulana Rajani Hassan Ali from Dar es Salaam expressed his regret and said that the services of late Muhammad Raza for the restoration of democracy and human rights are unforgettable. are And his death is very harmful for the organization of human rights. In the end, Maulana Rajani prayed to God Almighty and said, "O God, grant this deceased a place in His mercy, and give patience to the bereaved." Expressing his heartfelt condolences and sympathies to the bereaved and the family members, Rajani said that in this time of sorrow, we also share their grief.

  From Hasan Bhai. East Africa Tanznia Dar Es Salaam Cell No +255745344366 whatsaap +919998269850

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.