Habari za Punde

Bingwa wa ngumi za Wanawake Natasha Paula Jonas atangazwa Balozi wa Utalii

Waziri wa Utalii na mambo ya kale Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na waandishi wa Habari wakati akimtambulisha Bingwa maarufu wa ngumi za Wanawake Natasha Paula Jonas kuwa Balozi wa Utalii.
Waziri wa utalii namambo ya kale Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi cheti maalum Bingwa maarufu wa ngumi za Wanawake, Natasha Paula Jonas mara baada ya kumtangaza kuwa Balozi wa Utalii

PICHA NA FAUZIA MUSSA

Na Fauzia Mussa


Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imemtangaza Bingwa maarufu wa ngumi za Wanawake Natasha Paula Jonas kuwa Balozi wa Utalii

Akimtambulisha Balozi huyo kupitia vyombo vya habari Waziri wa Wizara hiyo Mhe Simai Mohammed Said amesema hatua hiyo inatokana na nafasi yake halisi ya michezo kimataifa katika ulimwengu wa ndondi

Amesema Natasha ambae pia ni mtangazaji wa kituo cha michezo cha sky sport ,ubalozi wake utasaidia kutangaza na kuwa kivutio kwa wageni zaidi na kuhamasisha kizazi kijacho katika kupenda michezo na kufikia adhma ya kukuza mtindo wa maisha katika kujishughulisha na michezo ya nguvu.

Mhe Simai amefahamisha kuwa katika kipindi chake kama Balozi atashiriki kikamilifu katika kampeni za uhamasishaji ,matukio ya michezo na shughuli za kujenga mahusiano na jamii pamoja na kutambulisha fursa za nafasi za vijana katika michezo.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo bi Fatma Mabrouk Khamis amesema wizara inakamilisha mpango mkakati ambao utawahusisha mabalozi katika shughuli mbali mbali na kusaidia kuhamasisha utalii kwa upande wa jamii

Nae bondia Natasha Paula Jonas ameahidi kuiunga mkono Zanzibar katika kuitangaza kupitia mchezo huo pamoja na kuendeleza mafunzo ya mchezo huo kwa vijana

Bondia Natasha amevutiwa na utamaduni, ukarimu na ushirikiano mzuri kutoka kwa wawazanzibari
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.