Habari za Punde

Mbunifu wa Mavazi Katona Kashona Kuzindua Tai Kirungu

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam. 
MBUNIFU wa mavazi nchini mwenye kufanya kazi za Sanaa ya ubunifu wa mavazi, Didas Katona akifahamika zaidi kama 'Katona Kashona', anatarajia kuzindua Tai kirungu ((Bow Tie), tukio litakalofanyika Agosti 4, ukumbi wa Club The Marz zamani Nyumbani Lounge. 

Katona Kashona amebainisha kuwa, tukio hilo watu mbalimbali maarufu wamealikwa huku burudani ya muziki wa 'live' ilitarajiwa kutolewa na Suk Mr Piano Man na DJ Jd.

"Habari Wanatanzania kwa mara nyingine tena nakuja kwenu kama Mtanzania mbunifu wa mavazi niliyefanya kazi na watu wengi wakiwemo maarufu, kwa kipindi hiki nakuja na Tai kirungu. " Amesema Katona Kashona. 

Na kuongeza kuwa, siku hiyo kutakuwa na 'displays'  ya midoli itakayo valia Tai na zitauzwa kwa wahitaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.