Habari za Punde

Elimu za Madrasah huwakuza watoto kimaadili na kiimani

Mwalimu Mkuu wa Almadrasatul-Shaafiiyya Islamiya Hussein Idd Salim akizungumza na uongozi wa Skuli ya Trifonia Academy walipofika Chuoni hapo katika ziara yao kuelekea kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake
Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Trifonia Academy wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Madrasatu Shaafiiyya Islamiya wakati walopowatembelea ikiwa ni miongoni mwa shughuli za kusherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa skuli hiyo.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO


Na Rahma Khamisi Maelezo    

 

Wadau mbalimbali chini wameombwa   kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa  na walimu wa madarasa ili kuwasaidia wanafunzi katika kukuza elimu ya kumtambua mola wao.

 

Wito huo umetolewa huko Madrasati Shafaia  Mwanakwerekwe na  Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Trifonia Idd Hussein Idd wakati alipotembelea  Madrasa hiyo ikiwa ni shamrshamra za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

 

Amesema wadau wengi wamejikita katika kusaidia mambo mengine ya kijamii na kuziacha Madrasa bila ya kuzipitia jambo ambalo si la kufurahisha kwani elimu zinazotolewa katika  madrasa hizo ni muhimu na zinasaidia kuwakuza watoto hao katika maadili mema  na kuwajenga  kiimani .

 

"Naiomba jamii na wadau wa elimu kujitokeza kuzisaidia Madrasa ambazo mazingira yake hayako vizuri ili kupata radhi za Mola wetu,"alisisitiza Mwenyekiti.

 

Nae Mwlimu Mkuu wa Skuli ya Trifonia  Protas  Bernado Nikodem amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza  , kuangalia mazingira ya madrasa hiyo na   kusaidia panapohitaji  msaada ili kuweka muzingira rafiki  ya kujifuniza  kwa  wanafunzi hao .

 

Aidha amefahamisha kuwa kazi ya waalimu wa Madasa ni kazi ya wiito, hivyo ipo haja ya  kuwaunga mkono kwa kuwapa mashirikiano ya hali ya juu ili kuendeleza kufanya kazi hiyo .

 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Madarasa hiyo Hussein Idd Salim  amesema madrasa hiyo ni mbovu  kwa muda mrefu sasa hali inayowakosesha amani na utulivu wa kusoma hasa katika kipindi cha mvua.

 

Aidha ameiomba Serikali kuzingatia muda  waasomo kwani wanafunzi wengi wanatoroka Madrasa  kwa kisingizio cha kwenda masomo ya ziada (tution).

 

Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu amewaomba wazazi na walezi kuongeza ushikiano kwani baadhi yao wanashindwa kuwasilisha michango kwa wakati jambo linapolekea kurudisha nyuma maenedeleo ya Madrasa hiyo.

 

Hata  hivyo amepongeza na kuushukuru Uongozi wa Skuli ya Trifonia kwa kufika katika madrasa yao   na kuwataka Skuli nyengine kuiga mfano huo ili kukuza elimu za vijana.

 

Matembezi hayo ni muendelezo wa ziara ya skuli ya Trifonia kupeleka mrejesho kwa jamii ikiwa ni  shamrashamra za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.