SERIKALI ya Mapinduzi ya
Zanzibar imesema daima inaungamkono jitihada za wadau wa mendendeleo nchini na kwamba
inathamini michango na huduma wanazozitoa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza
na wajumbe wa bodi na watendaji kutoka benki ya CRDB waliofika kumkabidhi mfano
wa Kadi ya benki ya Al barakaah ya CRDB.
Dk. Mwinyi aliipongeza benki hiyo kwa huduma wanazozitoa
kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla.
Pia aliwasihi kudumisha ushirikiano wao baina ya
sekta ya binafsi na taasisi za umma ili wapate mafanikio makubwa zaidi.
Rais Dk. Mwinyi aliishukuru benki hiyo kwa heshima
kubwa waliyompa kuwa mteja wao wa kunzwa kwa Zanzibar kupokea huduma za benki
ya Al barakaah.
“Natoa shukurani zangu kwa heshima kubwa mliyonipa,
hii ni shughuli ya kutoa kadi na ya kwanza mmenipa mimi” alishukuru Dk. Mwinyi.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliueleza uongozi wa benki
hiyo mwamba Serikali inaungamkono jitiha na huduma wanazozitoa benki hiyo kwa Zanzibar.
Pamoja na kuwapongeza kwa mafanikio makubwa waliyoyapata ndani ya kipindi
kifupi tokea kuanzisha huduma za Al barakaah kwa visiwa vya Unguja na Pemba.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa huduma
za benki za Kiislam za Al barakaah za CRDB, Abdul Van Mohamed, alisema benki
hiyo tokea imeanzisha huduma zinazofuata misingi ya Kiisslam (Al barkaah benki)
wamepata mfanikio makubwa ndani ya kipindi
cha miaka miwili.
“Hadi sasa tumefanikiwa kupata wateja zaidi ya 70,
000 kwa Tanzania nzima, tumetoa mikopo inayofuata sharia za dini ya kiislam
shilingi 87bil na tumefanikiwa kuhifadhi amana za wateja zinazosimamiwa kwa
misingi sharia shilingi bilioni 95 kwa nchi nzima” alifafanua.
Alisema CRDB imetoa mchango mkubwa kwenye ujumuishi
wa kifedha nchini pamoja na maendeleo ya kiuchumi kwa taifa na wananchi kwa
ujumla nakuongeza kuwa tokea kuanzishwa kwa huduma hizo nchini kumekuwa na
uhitaji mkubwa zimepokewa na wananchi kwa uitikio mkubwa.
Van alieleza CRDB Al barakaah kwa Zanzibar imekua na
mchango mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar na Wananchi wake kwa kuwapa huduma nyingi ikwemo mikopo ya uchumi
wa buluu, alisema zaidi ya bilioni 18 wamepewa wananchi wa Zanzibar kupitia
dirisha la Al barakaah benki pia masoko zaidi ya bilioni 10 yametolewa kupitia
dirisha hilo.
Aidha, alieleza benki hiyo ilifanikiwa kutoa mikopo inayofuata
sharia kwa wafanya biashara na waajiriwa wa Zanzibar zaidi ya bilioni 10, amana
za wateja zaidi ya bilioni 28 kwa zanzibar pekee, CRDB.
Akizungumzia mfano wa kadi za “Al barakaah benki” Mkuu
wa kitengo cha Al barakaah benki ya CRDB, Rashid Rashi alisema mwenekano wake
zinaendana na matakwa na matarajio ya wateja wao kwa kujua pesa zao zipo mikono
salama na uangalizi maalumu unaoendana na imaani na maadili ya sharia za wateja
wao.
Alisema kadi hizo zimeunganishwa na mifumo ya kimataifa inampa uhuru mteja
kufanya miamala sehemu yeyeote duniani za huduma za ATM , kwa upande wa Tanzania
alieleza kadi hizo zinauwezo wa kutumika kwenye ATM zisizopungua 600, mawakala
zaidi ya elfu 28 na matawi kwa Tanzania nzima zaidi ya 240.
Kwa upande wa Zanzibar alisema kuna matawi manne, wakala
zaidi ya 240 na ATM 19 kwa Unguja na Pemba ambako huduma za Al barakaah benki
zinapatikana.
Aidha, kwa tawi la Wete, Pemba, Mkuu kuyo alieleza
tokea lilipofunguliwa mwaka jana kutokana na maelekezo ya Rais Dk. Mwinyi, kwamba
benki hiyo ifungue tawi Wete ili iendeleze uchumi wa wananchi wa eneo hilo na
tokea ilipofunguliwa mwaka jana, tayari imefanikiwa kuwa na amana za wateja
shilingi bilioni 3.3, mikopo zaidi ya bilioni 2.7 na wateja zaidi ya 2,200.
Alisema amanda zote zimewekwa upande wa Sharia benki
kama mahitaji ya wateja wao yalivyo na kueleza kuwa imekua chachu kwa upande wa
Pemba.
Rais Dk. Mwinyi anakuwa mteja wa kwanza kwa Zanzibar kufungua hesabu ya benki ya Al barakaah ya CRDB pia ni wakwanza kupokea kadi ya ATM ili afurahie huduma hizo za benki hiyo.
No comments:
Post a Comment