Habari za Punde

Waziri Lela akutana na Balozi wa Marekani nchini

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa akifurahia jambo wakati alipokuwa akimkaribisha balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Michael Anthony Battle huko ofisi kwake Mazizini Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Michael Anthony Battle huko ofisi kwake Mazizini Unguja.
Katika mazungumzo hayo balozi Battle ameahidi kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa katika sekta ya Elimu.
Katibu mkuu wa wizara hiyo Bwana Khamis Abdulla Said alishiriki katika mazungumzo hayo leo tarehe 20/9/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.