Habari za Punde

Hafla ya Sherehe za Walimu Wilaya ya Magharib 'A' ya kutimia Miaka 16 tangu kuanzishwa Vituo vya (TUTU)
 Utowaji wa Elimu bora kwa wanafunzi wa Maandalizi na Msingi ndio msingi imara wa kuwaandaa wataalamu bora wa taifa la kesho.
Amesema hayo Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi Bi. Fatma Mode Ramadhani, wakati wa hafla ya Sherehe za Walimu Wilaya ya Magharib 'A' ya kutimia Miaka 16 tangu kuanzishwa Vituo vya (TUTU) Wilayani humo, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Walimu Bububu Unguja.
Amesema, Walimu wa (TUTU )wajitahidi kutoa taaluma iliyo bora kwa wanafunzi wa maandalizi na Msingi ili kuwajengea mazingira mazuri ya Msingi wa Elimu utakao weza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae pamoja na kuleta tija kwa taifa kwa jumla.
Aidha, Amewasihi Walimu hao kufanya kazi kwa bidii ili lengo la Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Uongozi wa Rais Mwinyi kuhusu uimarishaji wa ubora wa Elimu uweze kufikiwa.
Hata hivyo, ametoa wito kwa walimu Wakuu kuwasimia vyema walimu wa Vituo vya (TUTU) pamoja na kuwashirikisha katika Vikao rasmini vya skuli wanazo zisimamia kama walimu wengine.
Kwa Upande wake Mratibu wa Vituo vya (TUTU) Wilaya ya Magharib "A" Unguja Bi. Asha Muhamed Omar ameishukuru Wizara ya Elimu Zanzibar kwa kuvisaidia Vituo vya (TUTU) pamoja na kuimarisha miundo mbinu iliyo imara ili watoto waweze kusoma katika mazingira yaliyo bora.
Akisoma Risala kwa niaba ya Walimu wa Vituo vya Tusome Tujifunze (TUTU) Mwalimu Suhaila Mapunda Khamis amesema, ndani ya miaka 16 Wilaya ya Magharib "A" ni miongoni wa Wilaya 3 za mwanzo za uanzishwaji wa Vituo vya Tutu Zanzibar.
Amesema, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, Wilaya ya Magharib "A"inaongoza kwa watoto walio wengi wanaohitaji kupata elimu ikiwemo maadalizi, hivyo Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wilaya ya Magharib "A" ziliongeza Vituo vya (TUTU) kufikia 27 mwaka 2020 ikiwa na walimu 54 na Wanafunzi 2248.
Amesema, Watoto waliopita katika Vituo ni wengi na wapo walomaliza Vyuo Vikuu na wengine wameajiriwa Serikali ni na Sekta binafsi.
Amesema, ukuaji wa Mjini na Vijiji katika Wilaya hiyo pamoja na uandikishaji mkubwa wa wanafunzi, umepelekea uwepo wa kunachangamoto ya uhaba wa majengo pamoja na vyoo.Hivyo wameiomba Wizara ya Elimu kuzitatua changamoto hizo ili kuweza kuimarisha uboreshaji wa utowaji wa Elimu bora.
Imetolewa na kitengo cha habari na Mawasiliano (WEMA)
Tarehe : 30/09/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.