Habari za Punde

Kamanda Mallya -Awataka Wakristo kuwa Watoaji Kwenye Shughuli za Kimaendeleo

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Theopista Mallya ameongoza harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kununua gari aina ya Coaster kwaajili ya kwaya ya mtakatifu bikira maria kanisa la Parokia ya familia takatifu jimbo katoliki la Sumbawanga mtaa wa Majengo mjini Tunduma Mkoani Songwe.

Kamanda Mallya ameyasema hayo leo Oktoba 15, 2023 akiwa kama mgeni maalum katika harambee hiyo ambayo aliwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi  Milioni 23 kati ya Shilingi Milioni 50, zinazohitajika kwaajili ya ununuzi wa gari hilo pesa hizo ni pamoja na ahadi mbalimbali zilizotolewa na wageni waalikwa ikiwa ni pamoja na wanakwaya wa kanisa hilo.

Tukio hili limekuja baada ya juhudi  za kamanda wa polisi mkoa wa Songwe kuwa na muendelezo wa kutembelea nyumba za ibada ili kuhamasisha jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu kwa njia ya ubia endelevu.

Kwa upande wa wanakwaya hao wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada kubwa wanazozifanya kwa kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maswala ya kimaendeleo na wameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika himaya zao.

Toka dawati la habari mkoa wa Songwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.