Habari za Punde

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said Azungumza na Waandishi wa Habari. Uzinduzi wa Tamasha la pili la Z- Summit



Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuunga mkono jitihada mbali mbali za Wananchi, Wadau katika kuleta maenedeleo ndani ya sekta ya Utalii nchini.

Ameyasema hayo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea Uzinduzi wa Tamasha la pili la Z- Summit katika hoteli ya Golden Tulip Iliyopo Uwanja wa ndege Zanzibar .
Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Simai ameeleza kuwa Tamasha la Z- Summit lina mchango mkubwa katika sekta ya Utalii kwa Zanzibar, Tanzania na hata Ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Mhe. Simai amefafanua kwamba zaidi ya Wafanyabiashara 100 - 300 wakiemo mawakala kutoka nchi 17 hushiriki pamoja katika Tamasha hilo, hivyo hii ni hatua kubwa katika kukuza sekta ya Utalii nchini kwani mkusanyiko huo unaonyesha zaidi kishindo cha kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kujenga Uchumi imara wa bluu.
Aidha Mhe. Simai ametoa wito kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya Utalii nchini kuungana pamoja katika Tamasha hilo la pili ili kufaidika na fursa zilizomo ndani ya sekta ya Utalii, mashrikiano hayo yatapelekea kufanya kazi pamoja kuelekea malengo ya pamoja katika kuendesha sekta hiyo.
Nae Mwnyekiti wa Tamasha hilo ndugu Rahim Bhaloo ameishukuru sana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinachukuliwa na Wananchi katika kuinua sekta ya Utalii nchini.
Aidha amempongeza Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa Ushirkiano anaowapa kuanzia Tamasha la kwanza na hadi sasa hii inaonesha dhamira njema ya Serikali katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake .
Ndugu Rahim Bhaloo ametoa wito kwa vijana, wadau na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa zilizomo ndani ya sekta ya Utalii ili kuzidi kufaidika na maendeleo ya sekta ya hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.