Habari za Punde

Meli kubwa ya kitalii yatia Nanga Bandari ya Malindi leo


Meli kubwa ya ZUIDERDAM imetia nanga leo tarehe 14/11/2023 katika Bandari ya Malindi Zanzibar, akizungumza mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Zanzibar Nd. Rahim Bhaloo amesema kuwa meli hiyo iliyobeba jumla ya Watalii 1412 ilianza safari yake nchini Marekani na kupita Nchi mbali mbali duniani ikiwemo Portugal, Spain, Morocco, Tunisia, Creek Islands, Cyprus, Salala (Oman) Sychelles na hatimae leo kuwasili Zanzibar.


 Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said amethibitisha ujio wa Meli kubwa Kisiwani Unguja iitwayo ZUIDERDAM ambayo inatarajiwa kuwasili leo tarehe 14/11/2023 katika Bandari ya Malindi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kikwajuni Zanzibar Mhe. Simai ameeleza kuwa Meli hiyo kubwa yenye urefu wa mita 291 ilianza safari yake tarehe 10/10/2023 nchini Marekani na kupita Nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Portugal, Spain, Morocco, Tunisia Creek, Cyprus, Salala (Oman) Sychelles na hatimae kufika Zanzibar inatarajiwa kuja na idadi ya Watalii 1561 na Wafanyakazi 778 .
Amesema ujio wa Meli hiyo ni kufuatia maagizo ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhakikisha Utalii wa Meli unaimarishwa Visiwani Zanzibar.
Akitoa Ufafanuzi juu ya faida zitakazopatikana kwa ujio wa Meli hiyo Mhe. Simai ameeleza kuwa itaendelea kufungua milango kwa kampuni nyengine za Utalii wa Meli kuleta Meli zao Zanzibar jambo ambalo litazidi kuiweka Zanzibar katika Ramani ya Nchi au Visiwa ambavyo vinaendesha Utalii wa Meli yani ‘Cruise Tourism’ katika viwango vikubwa.
Mhe. Simai ametoa wito kwa Taasisi, Mashirika, Wanaotembeza Watalii (Tour Guider) na wanaoshughulika na Utalii pamoja na Wananchi wote kuwaonesha Ukarimu Wageni hao na kuwapa mashirikiano mazuri kwa tija ya Utalii wetu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.