RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipngeza Benki ya Dunia kwa
jitidaha zake za kuendelea kuziunga mkono Tanzania kupitia miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo,
Ikulu Zanznibar alipozungumza na Rais wa Benki hiyo, Ajay Singh Banga na ujumbe wake,
wanaotarajiwa kuhudhuria
mkutano wa 20 wa Mapitio ya benki hiyo, unaotarajiwa kufanyika, ukumbi wa Golden
Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar.
Dk. Mwinyi alimueleza mgeni wake huyo
juu ya Zanzibar inavyonufaika na fursa nyingi kutoka Benki ya Dunia, kupitia
miradi ya kimkakati ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji safi na utunzaji wa
mazingira, umeme vijijini ambayo inatekelezwa Tanzania Bara.
Pia, Rais Dk. Mwinyi alieleza Zanzibar
inavyonufaika na miradi ya huduma za jamii unayoungwa mkono na Benki ya dunia
ikiwemo miradi ya uzalishaji umeme, maji safi na salama, miundombinu, uwezeshaji
wa Wanawake, afya, elimu na Uchumi wa Buluu ambayo imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa.
Alisema, Zanzibar imekua na miradi
mingi ya maendeleo inayoungwa mkono na Benki ya Dunia kupitia ushirikiano mzuri
uliopo baina ya benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi alieleza fursa nyengine
ambapo Zanzibar inanufaika kutoka Benki ya dunia ni pamoja na kuwajengea uwezo Wanzania
kupitia mikutano ya kimataifa, warsha, makongamano pamoja na misaada ya kiufundi.
Mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, Rais Dk. Mwinyi
alitembelewa na Mwakilishi
Mkazi wa Benki hiyo, Nathan Balete anaeziwakilisha nchi nyengine tatu za Afrika mbali na Tanzania zikiwemo
Malawi, Zambia na Zimbawe.
Naye, Bw. Ajei Banga, alisifu juhudi za Rais Dk. Mwinyi kwa kuimarisha maendeleo na
huboresha huduma bora za jamii kwa wananchi
wake na kueleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na benki hiyo
ikiwemo Zanzibar.
Pia alisifu uzuri wa kisiwa cha
Zanzibar na ukarimu wa watu wake waliojikita kwenye kuendeleza maendeleo.
Kwa mara ya kwanza, Zanzibar inakua mwenyeji wa Mkutano
mkubwa duniani wa Benki ya Dunia utakaohudhuriwa na wageni mashuhuri akiwemo
rais wa Benki hiyo, Ajei Banga, mkutano huo pia unaotarajiwa kuhudhuriwa kati
ya wageni 300 hadi 350 wenye lengo la kufanya mapitio ya miradi inayoungwa mkono
na benki hiyo, pamoja na mambo mengine pia utaangalia namna bora ya
utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na namna ya kuongezwa fedha na ruzuku kwa miradi
itakayofanya vizuri zaidi kwa mataifa wanufaika.
Zanzibar pia inanufaika fursa za Benki ya
Dunia kupitia sekta ya nishati hususani umeme wa jua, upepo na gesi asilia.
No comments:
Post a Comment