SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar
imesema inathamini sana mchango wa fani za Wasanifu, Wahandisi na
Wakadiriaji Zanzibar kwenye utekelezaji wa mipango mikubwa ya Maendeleo hasa
miradi ya ujenzi.
Imesema itaendelea kuwahusisha kikamilifu kwenye utekelezaji wa
miradi mikubwa ya maendeleo kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji wa wataalamu
wa Kitanzania katika miradi endelevu ya kimkakati ya uwekezaji nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameyasema hayo alipozindua taasisi ya wasanifu, wahandisi na wakadiriaji Zanzibar, kwenye ukumbi wa
hoteli Verde, Mtoni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, kwa kiasi kikubwa Serikali ilijitahidi
kuzitumia kampuni za ndani kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali hasa wakati wa
utekelezaji wa miradi mikubwa ya fedha za UVICO zilitumika kampuni za ndani
(wazawa) kwa lengo la kuwajengea uwezo ili wapate miradi mikubwa zaidi. Pia,
Rais Dk. Mwinyi alieleza miradi yote ilikamilika kwa ufanisi hali ya juu zaidi.
Alisema, Serikali zote mbili za (SMZ) na (SMT) zinafanya
jitihada za makusudi kushirikisha taaluma hizo kwenye shughuli tofauti za
maendeleo, ikiwemo kuweka mazingira yanayowawezesha kujiajiri, kuhamasisha
utambuzi wa fursa mbalimbali kupitia rasilimali zilizopo nchini pamoja na
kutenga bajeti kwa ajili ya kufanikisha utafiti na ubunifu mbalimbali.
“Tunajua tunahitaji kushirikiana ili kufanikisha dhamira ya
Maendeleo Endelevu hususan fani hizi kutokana na umuhimu wake kwa ustawi wa
nchi yetu”. Alieleza Rais Dk. Mwinyi.
vilevile Dk. Mwinyi alieleza hizo ni uti wa mgongo wa shughuli
nyingi za uchumi wa nchi kwani zinabeba dhima ya shughuli-mama katika harakati
za kujenga, kuimarisha na kuendeleza maendeleo ndio maana Serikali inazipa
mazingatio makubwa.
Alisema Serikali pia imefungua njia kwa fani hizo kuwa na
uthubutu na kujiamini sambamba na kuwasihi wahandisi hao kuendelea kuongeza
juhudi ili kazi zao zizidi kuchangia kiasi kikubwa cha kuchochea ukuaji wa
uchumi wa nchi.
Dk. Mwinyi alisema Tanzania ni nchi inayoendelea na inajivunia
kufikia Uchumi wa Kati, kutokana na kuwa na miradi inayochangia zaidi pato la
Taifa, nyuma yake wakiwepo wenye fani za usanifu, uhandisi na ukadiriaji wa ujenzi.
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi alieleza, Serikali ya Zanzibar
kupitia Uchumi wa Buluu imeendeleza Sera ya kuajiri wasanifu, wahandisi na
wakadiriaji wazalendo ikiamini kuna wakandarasi wazuri na washauri elekezi
mahiri (wazawa) wenye uwezo mkubwa wa kufanyakazi za uhandisi kwa weledi
kupitia miradi mbalimbali waliyoitekeleza kwa ufanisi mkubwa ni kielelezo cha
kuaminika kwao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na
Uchukuzi, Dk. Khalid Salim Mohamed amesema Sekta ya majengo na ujenzi Zanzibar
iko kwenye mageuzi makubwa kwa kasi kubwa ya ujenzi inayoendelea nchi nzima
zikiwemo barabara za mijini na vijijini, ujenzi wa skuli za ghorofa maeneo yote
ya visiwa vya Unguja na Pemba, ujenzi wa hospitali kwa wilaya zote nchini ujenzi
wa nyumba za makaazi miundombinu ya maji safi na salama pamoja na umeme.
Alisema hatua hiyo inatokana na dhamira njema na maono ya Rais
Dk. Mwinyi katika azma yake ya kuibadilisha Zanzibar na mandhari na haiba nzuri
ya maendeleo endelevu.
Alizipongeza juhudi za wahandisi wote kwa ushiriki wa wao mkubwa
wa mageuzi yanayoendelea nchini chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi, kupitia sekta
ya ujenzi na miundombinu.
Alisema, maisha ya kila siku yanategemea mchango na ushiriki
mkubwa wa wahandisi.
Dk. Khalid alifafanua makaazi ya watu wanayoishi, ofisi na mawasiliano
yao, nishati za umeme, madaraja na barabara wanazozitumia, maji safi na salama na
shughuli zote za jamii zina mnasaba mkubwa na kazi za wahandisi.
Hivyo, alileleza kuundwa kwa taasii ya Wasanifu, Wahandisi na
Wakadiriaji Zanzibar ni kielelezo muhimu cha kukuza uwezo wao katika kuimarisha
sekta ya ujenzi kwa maendelo ya nchi.
Naye, Rais wa Taasisi ya Wasanifu Wahandisi na Wakadiriaji
Zanzibar, QS. Abduswamad Mohamed Mattar amesema taasisi hiyo ilimedhamiri
kufanya makubwa zaidi kama mchango wao kwa taifa na kuadhimia kuwa na wanachama
wengi ambapo kwa sasa kuna wanachama 192. Hivyo. Aliwashauri wataamu wa fani
hizo kuendelea kushirikaina na kujiunga kwa wingi wao ili kushajihishana zaidi.
Aidha, alieleza kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na
taaasiisi mbalimbali za ujenzi ndani na nje ya nchi ikiwemo kutayarisha mafunzo
nao kujifunza zaidi mageni wasiyoyajua sambamba na kusaini hati tofauti za
makubaliano kwa taasisi mbalimbali za wahandizi bara na visiwani.
IDARA YA MAWASILINO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment