Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Azindua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 kwa ajili ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano. Anayempokea ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi hiyo alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu wakati Makamu wa Pili wa Rais alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Uhamiaji alipotembelea banda la taasisi hiyo ya Muungano wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akiondoka mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwaaga wananchi mara baada ya kufungua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umefanikiwa katika nyanja mbali mbali ikiwemo utekelezaji wa masuali yaa Muungano,kuimarika kwa Utaifa , umoja, amani, utulivu na ukuaji wa kiuchumi kwa pande zote mbili za Nchi.

Ameyasema hayo wakati akizundua maonesho ya Biashara ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar- es- Salaam ikiwa ni katika shamra shamra za sherehe za miaka 60 ya Muungano.

Amesema kuwa Uwepo wa Muungano umepelekea kuimarika kwa  huduma za kijamii kwa pande zote mbili za Muungano kama vile Sekta ya Maji safi na salama, Afya, elimu, ustawi na maendeleo ya jamii, makazi na usafiri.

Mhe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa udugu wa damu na urafiki ambao umepunguza migawanyiko ya kijamii na kuondoa hisia za ukabila na ubaguzi miongoni mwa wananchi.

Mhe. Hemed ameeleza kuwa ustawi wa wananchi umeimarika na kukua kwa uchumi kulikotoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuwekeza katika pande zote mbili za Muungano katika sekta ya Viwanda, Hoteli na kilimo cha biashara jambo ambalo linachangia kuongeza ajira kwa wananchi .

Aidha Makamu wa Pili wa Rais amesema ufanisi na utowaji wa huduma kwa wananchi umeongezeka kutokana na kuwepo kwa Sera na miongozo inayorahisisha kuondoa changamoto za kiutendaji na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka watanzania  hasa wanafunzi waendelee kusoma na kujifunza mambo mbali mbali yahusuyo Muungano ili kupata ukweli na uhalisia wa Muungano ambao ni tunu kubwa kwa Taifa letu, sambamba na kuwataka kuendelea kuuenzi, kuulinda na kuudumisha Muungano ambao ni nyenzo muhimu ya utambulisho wa umoja wa Watanzania.

Nae Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Khamis Hamza Chilo akimuwakiliza Waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo Mhe Selemani Said Jafo amesema mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na Muungano ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa uchumi na huduma za kijamii kwa pande zote mbili za Muungano.

Naibu waziri Khamis amesema  hoja mbali mbali ambazo zilikuwa ni kero kwa pande mbili za Muungano zimetatuliwa na zilizobakia zinendelea kujadiliwa na hatimae zitapatiwa utatuzi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Aidha Mhe. Chilo amewataka Watanzania kuendelea kutunza Mazingira hasa vyanzo vya Maji kwa kuacha kufanya shuhuli za ukulima na ufugaji katika vyanzo vya maji safi na salama.

Mapema mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. EDWARD MPOGOLO akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa kufikia miaka 60 ya Muungano kumesababishwa na kuwepo viongozi mahiri wa pande zote mbili za muungano hivyo wananchi wana haki ya kujivunia kwani viongozi hao wanaendana na fikra na mawazo waliokuwa nayo waasisi wa muungano huu Mwalimu J.K. NYerere na Sheikh Abeid Amani Karume za kuwaletea wananchi maendeleo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Mapema makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar alitembelea mabanda mbali mbali ya Maounesho ya wafanya biashara na taasisi za serikali zinazohusiana na Masuala ya Muungano.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.