Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Afunga Kongamano la Mafunzo kwa Wajumbe wa SADCOPAC Zanzibar

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katikati akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wakiingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Golden Tulip kwa ajili ya kufunga Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Na Maelezo Zanzibar 19/04/2024

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Mjaliwa Majaliwa amewataka wataalamu wa Kamati za kuchuguza hesabu za Serikali kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapatiwa ili kuzuia mianya ya rushwa na kuongeza kasi ya uwajibikaji .

Ameyasema hayo huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe na wataalamu wa Kamati ya SADCOPAC.

Amesema endapo wataalamu hao watayatekeleza kwa vitendo mafunzo hayo malengo yaliyokusudiwa yatafikiwa na kuleta mafanikio makubwa na mageuzi katika utendaji.

Waziri Majaliwa amewasisitiza washiriki kuyatumia mafunzo hayo kuleta mabadiliko katika taasisi za umma na kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo.

Aidha ameeleza kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa wajumbe kuweza kusimamia misingi ya uwajibikaji na kuimarisha haki na utawala bora.

Kwaupande wake Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amewata wajumbe wa mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatiakana nchini na kuwaomba kuwa mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii wa Zanzibar watapofika nchini mwao pamoja na kusimamia vyema misingi ya uwajibikaji.

Nao washiriki wa Mafunzo hayo akiwemo Mohammed Ahmada Salum Mwakilishi wa Jimbo la Malindi na Haji Amour Haji Mbunge wa Jimbo la Pangawe wamesema mafunzo hayo yamewapatia fursa ya kujifunza njia na taratibu mbalimbali wanazotumia nchi jirani katika kuendesha fedha za umma.

Aidha wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo pamoja na kubadilishana uzoefu kati ya  nchi wanachama na kuahidi kuyafanyia kazi kama ilivyokusudiwa ili kupunguza wizi katika kusimamia miradi ya Serikali.

Kongamano hilo la siku mbili ambalo limeshirikisha nchi wanachama 16 ikiwemo Botswana, Zimbabwe, Burundi, Rwanda, Kenya, Zambia, Uswatin, Mozambique, Angola, Uganda, Congo, Comoro, Moritius, Afrika ya Kusini, Malawi, Lushoto na wenyeji wao Tanzania lilikuwa na kauli mbiu “ kujenga uwezo kwa Wajumbe wa Kamati za hesabu Umma (PAC) wataalamu wanaosaidia kamati na wasaidizi wasimamizi wa mali za umma na Kamati zinazofanana na hizo katika kukabiliana na rushwa, uwajibikaji na uwazi”.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (C A G)Dk Othman Abas Ali akitoa hotuba katika hafla ya Ufungaji wa Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.


Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akitoa Hotuba ya Ufungaji wa Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kushoto akikabidhiwa Vitabu na Mwenyekiti wa Sadcopac Warren Chishe Mwambazi katika hafla ya Ufungaji wa Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Badhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Ufungaji wa Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Badhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Ufungaji wa Kongamano la Mafunzo kwa Viongozi na Wajumbe wa SADCOPAC hafla iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.19-04-2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.