RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa
Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum, kwa kufiliwa na Mama yake
Mzazi Bi.Mtumwa Ali Salum, alipowasili katika viwanja vya Masjid Mamiali Saateni
Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024 na (kushoto kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa
Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika kubeba
jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa Naibu Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum, kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Maiti
iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu
katika Sala ya Maiti ya Marehemu Bi.Mtumwa Ali Salum. Mama Mzazi wa Naibu Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Othman Ame Chum(kushoto kwa Rais) ikiongozwa na Mufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,
iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-12-2024
na kuzikwa Kijijini kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuka na Waumini wa Dini ya Kiislamu
katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa
Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Ame Chum,(kushoto kwa Rais) ikisomwa
na Sheikh.Dr. Muhyddin Ahmad Khamis (Maalim Siasa) baada ya kumalizika kwa Sala
ya Maiti iliyofanyika katika Masjid Mamiali Saateni Wilaya ya Mjini Unguja leo
9-12-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Marehemu
Bi. Mtumwa Ali Salum, Mama Mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman
Ame Chum, maziko yaliyofanyika Kijijini kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati
Unguja leo 9-12-2024
No comments:
Post a Comment